Sababu saba mtifuano wa Simba, Coastal

Dar es Salaam. Klabu mbili kongwe hapa nchini, Simba SC ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga, zimeingia kwenye mgogoro mkubwa juu ya uhamisho wa beki kisiki chipukizi, Lameck Lawi. Simba iliitaka huduma ya beki huyo wa Coastal Union na kufuata taratibu zote, wakakubaliwa. Ikatakiwa ilipe kiasi fulani cha fedha kama ada ya…

Read More

120 kuliamsha Lugalo Open 2024

Wachezaji zaidi ya 120 wa gofu wanatarajia kushiriki katika mashindano ya wazi ya ‘Vodacom Lugalo Open 2024’. Mashindano hayo, yalioandaliwa na klabu ya Lugalo yatafanyika kwenye viwanja vya klabu hiyo kati ya Julai 5-7. Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo aliliambia Mwanaspoti, klabu zote za hapa nchini zimealikwa pamoja na wachezaji…

Read More

Mzambia kunogesha mbio za magari Tanga

DEREVA muongozaji (navigator) kutoka Zambia, David Sihoka ni mmoja wa magwiji wa mbio za magari  wa daraja la juu barani Afrika wanaotegemewa kunogesha mashindano ya mbio za magari ya Advent yatakayofanyika jijini Tanga katikati ya mwezi ujao. Sihoka, amekuwa akimuongoza dereva Muna Singh wa Zambia kwa zaidi ya muongo mmoja sasa, safari hii atakuwa na…

Read More

Caravans T20… Lions yawaliza Flashnet Strikers

ILIKUWA ni jioni njema kwa Park Mobile Lions baada ya ushindi mnono wa mikimbio 60 dhidi ya Flashnet Strikers katika mduara (oval) wa Leaders Club jijini, Dar es Salaam mwishoni mwa juma. Mohamed Jawad aliyetengeneza mikimbio 54 na Kashif Ahamed aliyepiga mikimbio 39 ndio walioibeba Lions kuelekea ushindi wao na kuifanya jioni ya Jumamosi kuwa…

Read More

Ishu ya Prince Dube, Azam FC ilivyomalizwa

BAADA ya sintofahamu ya muda mrefu hatimaye Prince Dube amemalizana ‘kiungwana’ na Azam FC kufuatia ‘ushauri mzuri’ kutoka ‘mtu yule yule’ aliyehusika kushauri kwenye sakata la Feisal Salum ‘Fei Toto’. Dube amemalizana kwa kulipa fedh alizotakiwa kuilipa Azam ili aende anakopataka, vinginevyo mambo yangekuwa magumu kwake na hata kwa klabu iliyohusika kumshawishi kuzingua katikati ya…

Read More

Singida BS yavuruga usajili Simba, yavamia Ivory Coast

SINGIDA Black Stars (zamani Ihefu), imeendelea kusuka kikosi kwa ajili ya msimu ujao ikielezwa imepora nyota wawili wa kigeni waliokuwa wakihusishwa na Simba, huku ikimalizana na makipa Metacha Mnata na Beno Kakolanya ambaye anaweza akapelekwa kwa mkopo Namungo. Singida iliyobadilishwa jina hivi karibuni na kuhamishia maskani mjini Singida kutoka Mbarali ilikokuwa wakati ikitumia jina la…

Read More

Kipa Azam afichua kinachombakiza Bara

KIPA wa Azam FC, Mohamed Mustafa amesema licha ya kuichezea Ligi Kuu Bara kwa miezi sita tu akiwa na kikosi hicho ila amevutiwa na jinsi mashabiki wanavyozipenda na kuzifuatilia timu wanazozipenda tofauti na mataifa mengine Afrika na ndio kubwa lililomfanya aamue kusalia na kikosi hicho kilichomtoa Al Merrikh. Mustafa alijiunga na Azam katika dirisha dogo…

Read More

Madina yupo tayari kwa vita Zambia

NYOTA wa timu ya taifa ya Gofu ya Wanawake ya Tanzania kutoka Arusha, Madina Idd amekuwa ni Mtanzania wa pili kuthibitisha ushiriki wa mashindano ya wazi ya ubingwa wa gofu yanayotarajiwa kupigwa mwisho wa mwezi huu kwenye viwanja vya Lusaka, Zambia. Madina amethibitisha jana kutoka klabu ya Gymkhana ya Arusha kuwa atakuwa miongoni mwa Watanzania…

Read More