Kocha wa zamani Simba, atua Pamba Jiji

KOCHA wa zamani wa klabu za Simba na Tabora United, Goran Kopunovic ametambulishwa rasmi kuwa Kocha Mkuu wa timu iliyopanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, Pamba Jiji akipewa mkataba wa mwaka mmoja. Akizungumza na Mwanaspoti, Meneja wa Pamba, Ezekia Ntibikeha amesema timu hiyo imempa Goran mkataba wa mmoja wenye kipengele kumuongeza iwapo atafanya kweli…

Read More

Aggy Simba, Dokta Moo wafungiwa Simba

Wanachama maarufu wa Simba, Agness Daniel ‘Aggy Simba’ na Mohamed Hamisi ‘Dk Moo’ wamefungiwa na Sekretarieti ya klabu hiyo kujihusisha na masuala yote ya timu hiyo kutokana na malalamiko mengi ya kimaadili. Sekretarieti ya Simba imewafungia wanachama hao  hadi pale Kamati ya Maadili itakavyoamua vinginevyo. Katika taarifa ya Simba  kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo…

Read More

Raja yamtibulia Nabi, yabeba taji kininja

UKISIKIA kunyang’anywa tonge mdomoni ndiko huku, baada ya Raja Casablanca kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco (Batola) uliokuwa unaonekana wazi upo mikononi mwa FAR Rabat inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi. Nabi na FAR Rabat waliongoza Ligi hiyo kwa muda mrefu kabla ya mambo kutibuka baada ya Raja kuanza kula viporo vyake…

Read More

Kwa Mkapa wapewa heshima ya VAR

Dar es Salaam. Baada ya Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kutangaza kuwa msimu ujao mechi za Ligi Kuu zitakuwa teknolojia inayomsaidia mwamuzi kufanya marejeo ya picha (Video Assistance Referee-VAR), Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Ally Mayai amesema Uwanja wa Mkapa umeteuliwa kuwa kituo maalumu cha mafunzo kwa Afrika. Mwigulu aliyasema hayo juzi Alhamisi, Juni 13, 2024…

Read More

Kina Pacome walivyozoa Sh7 bilioni Yanga

Dar es Salaam. Yanga wikiendi iliyopita ilifanya mkutano wake mkuu wa mwaka ambao ulipitisha matumizi ya bajeti ya msimu uliopita, lakini pia ukapitisha matumizi ya bajeti ya msimu ujao. Kama ilivyo kawaida ya Yanga kwa miaka ya hivi karibuni mambo yao yamekuwa yakifanyika kwa mpangilio mzuri, mkutano huu ulifana kama mingine ya hivi karibuni. Ulihudhuriwa…

Read More

Control namba yakwamisha kesi iliyodumu kwa siku 3,000

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imechukizwa na kitendo cha mtu anayehusika kutoa namba ya malipo (control number) kwa ajili ya mshtakiwa Dilipkumar Maganbai Patel, kulipa faini kuchukua mwezi mzima kutoa namba hiyo. Patel anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 58/2016 yenye mashtaka mawili likiwamo la kusafirisha vipande 17 vya kucha za…

Read More

Maxime amvuta Nizar Dodoma Jiji

BAADA ya Dodoma Jiji kufikia makubaliano na aliyekuwa Kocha wa Singida Black Stars, Mecky Maxime ili kuinoa timu hiyo msimu ujao, tayari amependekeza jina la Nizar Khalifan ili akawe msaidizi wake ndani ya kikosi hicho cha walima Zabibu. Mwanaspoti linatambua licha ya Maxime kutotangazwa hadi sasa ila tayari amesaini mkataba wa miaka miwili huku akiwa…

Read More

Zimamoto yabadili upepo ubingwa ZPL

UPEPO umebadilika baada ya Zimamoto kupata ushindi wa tatu mfululizo ndani ya Juni katika Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) na kuipumulia JKU inayoongoza msimamo wa ligi hiyo kwa muda mrefu, zikitenganishwa kwa pointi moja tu kwa sasa, huku zikisalia mechi za raundi mbili tu kufunga msimu. Ushindi huo wa juzi uliopatikana kwenye Uwanja wa Mao…

Read More