Biashara, Tabora Utd lazima kieleweke

Kesho itajulikana ni nani atacheza Ligi Kuu Bara msimu ujao kati ya Biashara United ya Mara na Tabora United, ambazo zitamenyana katika mchezo wa marudiano kuwania kucheza ligi hiyo, kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kuanzia saa 10:00 jioni. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Karume, Musoma, wenyeji Biashara United walishinda…

Read More

Ahmad, Prisons ndo basi tena, Makatta kumrithi

WAKATI Tanzania Prisons ikithibitisha kocha Ahmad Ally, amevunja mkataba, muda wowote Maafande watamtangaza Mbwana Makata kuiongoza timu hiyo msimu ujao wa mashindano. Ally aliyejiunga na Prisons kwa mkataba wa miaka miwili tangu Novemba 2023 akichukua nafasi ya Fred Felix ‘Minziro’ na aliikuta timu nafasi ya 14 kwa pointi 13 na kumaliza msimu nafasi ya tisa…

Read More

Dortmund yamtema kocha Terzic | Mwanaspoti

DORTMUND, UJERUMANI: BORUSSIA Dortmund imetangaza kuachana na kocha Edin Terzic baada ya pande mbili kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba. Jambo hilo limetokea ikiwa umepita muda usiozidi wiki mbili tangu Dortmund ilipocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuchapwa mabao 2-0 na Real Madrid kwenye kipute kilichofanyika Wembley. Hata hivyo, pande hizo mbili zimefikia makubaliano…

Read More

Mkwabi avunja ukimya Simba, afichua shida iliopo

WAKATI hali ya sintofahamu ikiendelea ndani ya Simba ikiwamo kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi, Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Swedi Mkwabi  amevunja ukimya na kusema kinachoenelea sio sahihi na kuwataka viongozi wote kukaa chini na kumaliza tofauti zao ili kujenga umoja. Hivi karibuni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba akiwamo mwenyekiti wake, Salim…

Read More

Farid: Huyu Gamondi ni masta

KIRAKA wa Yanga anayemudu kucheza kama winga na beki wa kushoto, Fardi Mussa amekiri Kocha Miguel Gamondi anastahili jina la Masta, kwani hana mchezo kabisa na amekuwa akiwasapraizi wachezaji kila inapokuja mechi kiasi mchezaji anayeharibu huwa inakula kwake mazima. Farid anafichua Gamondi yupo tofauti na Nasreddine Nabi aliyeinoa timu hiyo kwa miaka miwili na nusu…

Read More

TFF yakunjua makucha Ligi Kuu ya Wanawake

TIMU ya Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), Ceasiaa Queens imelimwa faini ya Sh 2 milioni na baadhi ya maofisa na wachezaji wa timu hiyo kuadhibiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuvunja pambano la ligi hiyo iliyokuwa imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Alliance Girls. Pambano hilo lililopigwa Juni 11, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,…

Read More

Kama vipi… Kombe la Kagame lichezwe nyumbani, ugenini

MASHINDANO yaliyoboreshwa na kuongezwa ukubwa ya Klabu Bingwa ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Marekani mwakani, yameingia dosari baada ya klabu na ligi kuyapinga na kutishia kwenda mahakamani kwa hoja kuwa yanaongeza idadi ya mechi zinazovuruga ligi za nchi wanachama na pia kuweka rehani afya za wachezaji. Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) limeboresha mfumo na ukubwa…

Read More

Kagera Sugar inataka wapya 10

KAGERA Sugar inajipanga kuboresha kikosi chake kwa kupitisha panga kali ili kufanya vizuri msimu ujao, huku benchi la ufundi chini ya Fredy Felix ‘Minziro’ likipendekeza kuletewa wachezaji wapya 10. Timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 10 msimu ulioisha ikivuna pointi 34, huku ikilazimika kufanya maajabu katika mchezo wa mwisho kwa kushinda ugenini dhidi ya Singida…

Read More