Conte amewasikia, atuma salamu ya kibabe

KUMEKUWA na mijadala mbalimbali juu ya kiwango cha kiungo mkabaji mpya wa Yanga, Balla Mousa Conte aliyetua klabuni hapo kutoka CS Sfaxien ya Tunisia, lakini kumbe mwenyewe amesikia kila kitu kinachoendelea na kuamua kutoa kauli ya kibabe akituma salama mapema. Kiungo huyo amesema licha ya presha kubwa ndani ya kikosi hicho hasa eneo analocheza hana…

Read More

Jeshini kuna vita ya majirani CECAFA Kagame Cup

MIAMBA miwili ya soka la Sudan na Somalia, Al-Hilal Omdurman na Mogadishu City, itakuwa vitani leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, kutupa karata zao za kwanza katika mashindano ya Kombe la Kagame. Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana kwenye michuano hiyo mikongwe ya klabu za Afrika Mashariki na Kati,…

Read More

Maximo aanza Kagame Cup 2025, APR kicheko

KMC inayonolewa na kocha Marcio Maximo imeanza vyema michuano ya Kombe la Kagame 2025 kwa kuifumua Mlandege ya Zanzibar kwa mabao 3-2. Ushindi huo umeifanya KMC kuwa timu ya kwanza Bara kuzoa pointi zote tatu, baada ya jana Singida Black Stars kubanwa na Coffee ya Ethiopia iliyomaliza pungufu na kutoka suluhu jana kwenye Uwanja wa…

Read More

Kipagwile ajishtukia Dodoma Jiji | Mwanaspoti

MFUNGAJI namba mbili katika kikosi cha Dodoma Jiji kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliopita 2024-2025, Idd Kipagwile, amesema anajiona ana deni kubwa ndani ya kikosi hicho. Kipagwile anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara, alifunga mabao saba na asiti nne akizidiwa bao moja na Paul Peter aliyekuwa kinara wa ufungaji kikosini…

Read More

Maseke apewa miwili Coastal Union

TIMU ya Coastal Union imeendelea kuboresha kikosi chake kwa ajili ya kufanya vizuri msimu unaoanza Septemba 17, ambao mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chanzo cha uhakika kililiambia Mwanaspoti, uongozi wa timu hiyo umemsainisha kipa Wilbol Maseke mkataba wa miaka miwili, ukiamini uzoefu wake utakuwa…

Read More

Bocco alamba shavu jeshini | Mwanaspoti

NAHODHA wa zamani wa Simba na Taifa Stars, John Bocco aliyekuwa akikipiga JKT Tanzania katika Ligi ya msimu uliopita, amedaiwa kulamba shavu jipya kwa maafande hao, licha ya kwamba hatakuwa na kikosi hicho katika Ligi Kuu msimu wa 2025-26. Bocco aliyejijengea heshima akiwa na Azam FC aliyoipandisha Ligi Kuu mwaka 2007 na kutwaa nayo mataji…

Read More

Datius ajipa tumaini Mtibwa | Mwanaspoti

BAADA ya kupewa miaka miwili na Mtibwa Sugar, beki wa kulia Datius Peter amesema klabu hiyo itafufua matumaini mapya kwake ya kuendeleza kipaji alichonacho kwa kucheza soka la ushindani. Peter alijiunga na Mtibwa katika dirisha la usajili kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Kagera Sugar aliyodumu nayo tangu mwaka 2022, ambapo ameiacha baada ya kushuka…

Read More

Straika Kagera atimkia Kenya | Mwanaspoti

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Kagera Sugar raia wa Cameroon, Moubarack Amza amekamilisha usajili wa kujiunga na Bandari FC ya Kenya, itakayocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Yanga katika kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ Septemba 12. Nyota huyo atacheza dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, katika tamasha la kikosi hicho…

Read More

Adam apigia hesabu mpya Tabora United

MSHAMBULIAJI wa Tabora United, Adam Adam amesema mashindano ya Tanzanite Pre-Season International Tournament yaliyoandaliwa na Fountain Gate na kufanyika kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara, yanawasaidia kuwaweka tayari kimwili na kimbinu kwa ajili ya hesabu mpya za msimu wa Ligi Kuu Bara inayotarajia kuanza Septemba 17. Nyota huyo wa zamani wa Azam, Tanzania…

Read More