TETESI: Kapombe, Singida BS bado kidogo

UONGOZI wa Singida Black Stars (zamani Ihefu) inadaiwa umeanza mazungumzo ya kumpata beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe kwa lengo la kuwaongezea nguvu kwa msimu ujao wa mashindano. Kapombe aliyeichezea Simba kwa misimu saba mfululizo tangu aliposajiliwa 2017-2018 akitokea Azam FC sambamba na nahodha John Bocco, Erasto Nyoni na kipa Aishi Manula, ni mmoja…

Read More

TWFA Mwanza yapata mabosi wapya

SOPHIA Tigalyoma amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA) Mkoa wa Mwanza akimbwaga aliyekuwa mtetezi wa kiti hicho Sophia Makilagi. Tigalyoma amerejea kwenye nafasi hiyo tena baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo uliofanyikwa leo Jumamosi kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuanzia saa 4:00 hadi 4:50 asubuhi kwa…

Read More

RIPOTI MAALUM: Janga, Kwa nini kamari zinaongezeka licha ya athari mbaya? – 2

KATIKA mfululizo wa ripoti maalumu hii juu ya uraibu wa michezo ya kamari nchini, tuliona namna watoto wenye umri chini ya miaka 18 wanavyojiingiza, licha ya kuwepo kwa sheria kali zinazowazuia kujihusisha nayo. Tuliona namna watoto hususan wanafunzi wanavyotumia fedha wanazopewa na wazazi ili kutumia shuleni wakiziteketeza kwenye mashine za kamari maarufu kama Dubwi kwa…

Read More

Matawi Simba waitana fasta kujadili waliojiuzulu

SAA chache tangu uongozi wa Simba kutangaza mabadiliko makubwa, huku baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Msimbazio wakiachia ngazi, viongozi wa matawi wa klabu hiyo wameitana fasta ili kukutana kwa lengo la kujadili kilichotokea. Simba ambayo ina misimu mitatu mfululizo ikicheza Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho bila kubeba ubingwa,…

Read More

Metacha atua rasmi  Singida Black Stars

DILI limetiki. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mabosi wa Singida Black Stars (zamani Ihefu) Uongozi wa Ihefu, umemalizana na kipa Metacha Mnata aliyekuwa Yanga na muda wowote kuanzia sasa inatarajia kumtambulisha rasmi. Kipa huyo wa zamani wa  Azam, Mbao na Singida Big Stars, alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara…

Read More

Tanzania majanga, yaikosa Riadha Afrika

HUWEZI kuamini, lakini ndo ukweli ulivyo, kwa mara ya kwanza Tanzania haitashiriki mashindano ya Riadha Afrika (African Athletics Championship) tangu yalipoanzishwa mwaka 1979 baada ya wanariadha waliotarajiwa kubeba bendera kukosa vigezo vya ushiriki. Mashindano hayo ya 23 kwa mbio za viwanjani yafanyika kati ya Juni 21- 26, jijini Douala huko Cameroon, ikitazamiwa kushirikisha wanariadha zaidi…

Read More

Mbili zapanda Ligi Kuu Zenji, Zimamoto yaua

WAKATI maafande wa KVZ na Zimamoto wakifanya mauaji katika mechi za Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) iliyopo ukingoni, timu za Muembe Makumbi na Inter Zanzibar zimekuwa za kwanza kupanda ligi hiyo kwa msimu ujao wa 2024-2025. Muembe Makumbi ilikata tiketi ya kucheza Ligi Kuu kwa msimu ujao baada ya juzi kuifumua New King kwa mabao 2-0…

Read More

Mbappe hakanyagi nyasi za Santiago Bernabeu kifua mbele

INATAJWA Dennis Bergkamp alipokuwa usajili wa kwanza wa Kocha Bruce Rioch kila kitu kilibadilika Arsenal. Superstaa alikuwa amefika klabuni. Umri ulikuwa sahihi. Jina lilikuwa kubwa. Ulikuwa mwanzo mpya wa Arsenal mpya. Wachezaji wengi wakubwa wakatamani kucheza Arsenal. Kucheza kando ya fundi Dennis. Alitokea Inter Milan. Kabla ya Inter Milan alikuwa Ajax. Mchezaji mkubwa aliamsha ari…

Read More

Taifa Stars ipo tayari kuivaa Zambia

TAIFA Stars jana ilijifua kwa mara ya mwisho katika kujiandaa na mchezo wa tatu wa kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Zambia utakaopigwa Jumanne, huku mastaa karibu wote wakionyesha wanaitaka mechi hiyo itakayopigwa ugenini. Jana asubuhi kikosi hicho chini ya makocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ na Juma Mgunda kilipiga tizi…

Read More