Mshery arusha taulo Yanga | Mwanaspoti

BAADA ya kuitumikia Yanga kwa misimu mitatu ya mafanikio kipa namba mbili wa timu hiyo nyuma ya Diarra Djigui, kipa Abuutwalib Mshery imedaiwa ameomba kuondoka kusaka timu ambayo itampa nafasi ya kucheza ili kujihakikishia namba timu ya taifa, Taifa Stars. Mshery alijiunga na Yanga, Desemba 2021 hivyo ameitumikia timu hiyo kwa misimu mitatu yenye mafanikio…

Read More

Beki Mcolombia Azam amwibua Morris

NAHODHA wa zamani wa Azam FC, Aggrey Morris ameshindwa kujizuia kwa kuwapa tano mabosi wa klabu kwa kufanya usajili mzuri ulioibeba timu hiyo katika msimu wa mashindano wa 2023-2024 huku akimtaka beki Mcolombia, Yeison Fuentes (22) aliyemchambua na kusema amekamilika kwa kila idara. Azam ilimsajili beki huyo wa kati kwa mkataba wa miaka mitatu, akitokea…

Read More

Viunzi vinne kocha mpya Simba SC

Simba ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Kocha Steve Komphela (56) kutoka Afrika Kusini ili arithi mikoba ya iliyoachwa na Mualgeria Abdelhack Benchikha siku chache kabla ya msimu kumalizika. Kama kila kitu kitaenda sawa basi Komphela atatambulishwa kuwa kocha mkuu wa Simba kwa msimu ujao wa 2024/2025, licha ya kwamba anapingwa na baadhi ya viongozi…

Read More

Aubin Kramo arejea Asec Mimosas

WINGA Aubin Kramo wa timu ya Simba aliondoka nchini mwanzoni mwa wiki hii kwenda Ivory Coast ambapo akiwa huko amekuwa akifanya mazoezi na Asec Mimosas  aliyowahi kuic hezea kabla ya kutua Msimbazi. Kramo na mastaa wengine wa Simba ambao hawapo katika timu za taifa walipewa mapumziko ya siku 20 kabla ya kurejea kambini kujianda na…

Read More

Mo afanya mabadiliko makubwa Simba, Barbara ndani

KUNA kitu kinaendelea ndani ya Simba usiku huu. Huenda kufikia kesho yakatokea mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa juu. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Rashid Shangazi wamegomea uamuzi wa Rais wa heshima wa klabu hiyo akiwataka waandike barua ya kujiuzulu. Rais wa heshima…

Read More

Wajumbe wote wa MO wajiuzulu, Barbara aula Simba

WAJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba wameridhia uamuzi wa Rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewj ‘MO’ akiwataka waachie ngazi. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti viongozi wote wa bodi ya Simba wametii wito wa kiongozi wao ambaye ndiye aliyewateua. “Hadi sasa wajumbe wote  wamejiuzulu kama mambo…

Read More

Ouma aachiwa msala wa CAF

MABOSI wa Coastal Union wameamua kumuachia msala wote wa michuano ya kimataifa msimu ujao, kocha mkuu David Ouma aliyeiwezesha timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne ya Ligi Kuu Bara na kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, huku ikimshukuru na kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya. Wagosi wa Kaya hao wanarejea katika michuano ya kimataifa…

Read More

TFF yamgomea Samatta kutundika buti timu ya Taifa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limekiri kupokea barua ya kutaka kujiuzulu kwa nahodha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ‘Samagol’, lakini imemkaushia kwamba hadi watakapofanya kikao cha pamoja ili kujadiliana naye. Kabla ya TFF, kutoa msimamo huo, Mwanaspoti liliandika mapema wiki iliyopita kuhusiana na hatua ya Samatta kuandika barua, ambapo baba mzazi wa…

Read More

Sports inahitaji nyota saba tu!

BAADA ya kurejea katika Ligi ya Championship, African Sports ‘Wana Kimanumanu’ wameweka bayana kwamba wanahitaji wachezaji saba tu ili kuimarisha kikosi hicho kabla ya kuanza kwa ligi hiyo kwa msimu ujao. Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania kupitia Ligi Kuu ya Muungano mwaka 1988, wameweka mipango hiyo ikiwa ni mwanzo wa maandalizi ya kujiandaa na…

Read More

Adam apewa mwaka Azam FC

Azam imemsainisha mkataba wa mwaka mmoja, mshambuliaji Adam Adam, ambaye msimu ulioisha alimaliza na mabao saba, akiwa na Mashujaa FC na muda wowote kuanzia sasa itamtambulisha rasmi. Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ imeelezwa ndiye aliyesimamia dili lake, ndani ya mkataba huo kukiwa na sharti moja. Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliliambia…

Read More