
JICHO LA MWEWE: Taifa Stars ya Lunyamila na nidhamu ya Tshabalala
WIKI moja tu iliyopita chupa zilikuwa mezani stori zikiwa mdomoni. Nilikuwa na Edibily Jonas Lunyamila baa fulani Mbezi Beach tukipiga stori za zamani. Bahati iliyoje. Huyu ndiye wale kina Diego Maradona wa soka letu. Unamkumbuka Edibily? Alikuwa zaidi ya hatari ya kawaida. Winga aliyekuwa mbele ya muda. Mpira aliokuwa anacheza wakati huo kama winga tumekuja…