Uchaguzi ni kama dabi ya Kariakoo
Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 unakuja kwa kasi, na kama kawaida. Maandalizi yamejaa maneno, porojo na hekaya za kila namna. Mtaani tunapishana na mabango, bendera, fulana, khanga na kofia za wagombea. Kwa kawaida kampeni ni kachumbari ya uchaguzi. Kila chama kikipiga tantalila zake, kila mwanasiasa akijiona kuwa staa wa siasa. Na wapiga kura wanamshangilia kama…