
Mazito yabainika viwanja 14 vya Ligi Kuu, Kwa Mkapa…
UBORA wa viwanja una nafasi kubwa ya kuzalisha ligi, wachezaji na timu bora na ni jambo lililo wazi hakuna nchi yoyote iliyopiga hatua kisoka ambayo haina viwanja. Katika kuonyesha umuhimu wa uwanja katika mchezo wa soka, umewekwa kama sheria namba moja kati ya 17 za soka na hakujawahi kuwa na mabadiliko yaliyowahi kuifanya iwe tofauti…