KMC sasa yakubali yaishe Bara

KIPIGO cha bao 1-0 ilichopewa na Simba katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa jana jijini hapa kutokana na bao la mapema la Saido Ntibazonkiza, limelifanya benchi la ufundi la KMC kukiri mambo yamewatibukia na sasa wanapambana kumaliza nafasi ya tano katika msimamo wa ligi hiyo. KMC ilikuwa ikiwania nafasi ya nne ili ikate tiketi…

Read More

Kipa Mnigeria ampa tuzo Aziz Ki

KIPA wa Tabora United, John Noble ameshindwa kujizuia na kuweka bayana kwa mtazamo wake Kiungo Bora kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara ni Stephane Aziz KI na kutoa sababu za kumpa tuzo nyota huyo wa Yanga anayeongoza kwa mabao akilingana na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC. Kipa huyo aliyetunguliwa mara mbili msimu…

Read More

Dodoma Jiji yaua, Prisons sasa uhakika

MAAFANDE wa Tanzania Prisons imejihakikisha kusalia katika Ligi Kuu Bara baada ya leo kupata sare ya 2-2 ikiwa ugenini mbele ya Namungo na kutuliza presha za mashabiki ambao mwanzoni mwa msimu waliishi kwa mawazo kutokana na timu kufanya vibaya. Matokeo hayo yameifanya Prisons kufikisha pointi 34 na kusalia nafasi ya tano nyuma ya KMC, hivyo…

Read More

Aziz KI: Ishu ya mkataba mpya nawaachia Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI amesema kuhusu suala la kuongeza mkataba mpya ishu hiyo anaichia timu hiyo ambayo ameitumikia kwa msimu wa pili. Aziz KI hadi sasa analingana mabao na Feisal Salum kwenye vita ya ufungaji katika Ligi Kuu Bara kila mmoja akiweka kambani mabao 18. Akizungumza baada ya timu hiyo kukabidhiwa Kombe la Ligi…

Read More

Fei Toto awahenyesha mashabiki wa Yanga kwa Mkapa 

WAKATI Yanga ikiwa uwanjani ikipambana na Tabora United, mashabiki wa timu hiyo walikuwa kwenye presha kubwa iliyotokana na kiungo wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’. Presha ya mashabiki wa Yanga ilitokana na kufuatilia kwao mchezo wa Azam FC na Kagera Sugar uliokuwa unapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex,  ambao Fei Toto alikuwa tayari amefunga mabao mawili….

Read More

Yaliyojiri mzunguko wa 29 Ligi Kuu Bara

Yanga imekabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa staili ya aina yake kwa kombe hilo kushushwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jana kwa chopa, tukio ambalo halikuwahi kufanyika katika ligi hiyo misimu iliyopita, huku ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tabora United. Tukio hilo hapana shaka ndilo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu…

Read More

Coastal Union yakata tiketi CAF

WAGOSI wa Kaya, Coastal Union wamejihakikisha nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao baada ya leo kukata tiketi ya CAF kwa kutoka suluhu na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, kwani sasa imefikisha pointi 42 ambazo haziwezi kufikiwa na KMC iliyokuwa ikiifukuzia iliyo na pointi 36 na hata kama zitashinda mechi za…

Read More

Geita Gold hali tete Ligi Kuu

WACHIMBA Dhahabu wa Geita, Geita Gold, wameendelea kujiweka pabaya katika Ligi Kuu Bara baada ya leo kufumuliwa mabao 2-1 na Singida Fountain Gate kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na sasa watalazimika kushinda mechi ya Jumanne mbele ya Azam iwapo hawataki kushuka daraja moja kwa moja. Geita ipo nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na…

Read More

Mtibwa Sugar yaaga rasmi Ligi Kuu Bara

MABINGWA wa zamani wa Tanzania msimu wa 1999 na 2000, Mtibwa Sugar imeshuka rasmi jana baada ya kufumuliwa mabao 3-2 na Mashujaa katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Mtibwa iliyoanzishwa mwaka 1988 na kupanda Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu) 1996, imeshuka kutokana na kusaliwa na pointi 21 ikiwa na…

Read More