Saido atumia siku 150 kumpindua Baleke Simba

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ametumia siku 150 kumpindua aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Jean Baleke katika ufungaji wa mabao ndani ya timu hiyo baada ya kufunga mawili katika ushindi wa 4-1, dhidi ya Geita Gold. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi jana, Saido alifunga…

Read More

Ki, Fei wairudia bato ya Mayele na Mpole

BATO ya ufungaji wa mabao ya Ligi Kuu Bara, baina ya viungo Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC, inaweza ikajirudia ilivyokuwa katika  msimu wa 2021/22 kati ya  George Mpole na Fiston Mayele anayeichezea Pyramids ya Misri kwa sasa. Katika msimu wa 2021/22, Mayele akiwa Yanga na Mpole alikuwa…

Read More

Ifahamu asili ya hat trick

KATIKA fainali za 22 za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka juzi, wachezaji wawili Concalo Ramos wa Ureno na  Kyllian Mbape wa Ufaransa ndio walioibuka na kile ambacho kwa kimombo kinaitwa hat trick yaani kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja. Hawa wawili wameifanya idadi ya wachezaji kufunga hizo hat trick kufikia 54 katika michezo zaidi…

Read More

Makipa watavyoiweka katika wakati mgumu Stars kuelekea AFCON

IMESALIA miezi saba kabla ya kufika mwaka 2025 ambapo Tanzania itashiriki fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco. Tanzania ni miongoni mwa timu nane zilitakazo cheza michuano hiyo ikiwemo Somalia, Djibouti, Sao Tome, Chad, Mauritius, Sudan Kusini, Liberia na Eswatini. Asilimia kubwa ya wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ina mabeki wengi wenye…

Read More

Simba yafika bei kwa Mzamiru

SIMBA imeshtuka hii ni baada ya kuamua kumuita kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin haraka kwa ajili ya makubaliano ya mkataba mpya baada ya baadhi ya timu kuonyesha nia ya kumhitaji. Kiungo huyo ambaye amehudumu kwa muda mrefu ndani ya kikosi cha Simba alikuwa anawindwa na Azam FC sambamba na Ihefu FC, timu ambazo zilikuwa zinataka huduma…

Read More

Saa saba za Boka, Yanga mezani bila matumaini

DILI la Yanga na beki Chadrack Boka wa FC Lupopo limeingia ugumu baada ya pande zote mbili kukaa mezani kwa saa saba bila kufikia muafaka. Mwanaspoti limejiridhisha kwamba bosi wa nyota huyo, Jacques Kyabula Katwe alitua Dar es wikiendi iliyopita kwa ndege binafsi pamoja na ishu zake binafsi, lakini pia alikuja kukamilisha dili hilo. Lakini…

Read More

Adam afunguka kilichomng’oa Mashujaa | Mwanaspoti

MUDA mchache baada ya uongozi wa Mashujaa FC kuweka bayana kuachana na kinara wa mabao wa timu hiyo, Adam Adam  mchezaji huyo amevunja ukimya na kufunguka kilichomng’oa. Mshambuliaji huyo mwenye mabao saba katika Ligi Kuu ambaye mkataba alionao na klabu hiyo unaisha mwisho wa msimu huu, ameliambia Mwanaspoti  ameachana na timu hiyo baada ya kuomba…

Read More

Aziz KI ampindua Fei Toto, afikia rekodi ya Mayele

MABAO mawili aliyofunga kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki katika ushindi wa wa 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji yamemfanya kufikisha 17, hivyo kuwa kinara akimpiku nyota wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ mwenye 16. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Aziz Ki amefunga mabao hayo…

Read More

Fainali FA kupigwa New Amaan Stadium, Zanzibar

Mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) kati ya Yanga dhidi ya Azam FC sasa utapigwa Juni 2, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar badala ya ule wa Tanzanite ulioko Babati, Manyara. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa hiyo ambayo uamuzi wa kubadilisha uwanja umefanywa na kamati ya utendaji ya shirikisho…

Read More