Simba, Yanga, Azam na Singida kuanzia ugenini

DROO ya michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu ujao tayari zimemalizika, ikishuhudiwa miamba ya soka nchini Yanga, Simba, Azam FC na Singida Black Stars zikipangwa kuanzia ugenini. Mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na watani zao Simba iliyomaliza nafasi ya pili…

Read More

Kocha Uganda achekelea ushindi wa kwanza

FURAHA na shangwe zilitawala kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Namboole, Kampala baada ya Uganda Cranes kupata ushindi wao wa kwanza kwenye michuano ya CHAN 2024, wakiiadhibu Guinea mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa Ijumaa usiku. Bao la kwanza la Uganda lilifungwa dakika ya 31 na Regan Mpande, aliyetumia vyema krosi na kuupiga kichwa kilichomshinda kipa wa…

Read More

Joaquim Paciencia ndiye mkali wao

WAKATI zikiwa zimeshachezwa mechi 12 (kabla ya zile za jana) nyota wa Angola, Joaquim Paciencia ndiye mchezaji aliyefunga bao la mapema zaidi katika michuano ya CHAN 2024 inayoendelea katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zilizoandaa kwa pamoja. Straika huyo anayeitumikia klabu ya Bravo do Maquis, alifunga bao dakika ya saba alipoitanguliza Angola mbele ya…

Read More

Straika Algeria auota ubingwa CHAN 2024

MSHAMBULIAJI nyota wa Algeria, Aimen Mahious, ameweka wazi dhamira yake ya kuiongoza timu yake kutwaa ubingwa wa CHAN 2024, akisisitiza kuwa huu ndio wakati wao wa kutimiza ndoto hiyo. Katika mahojiano maalum na mtandao wa CAF, Mahious amefunguka kuhusu maumivu ya fainali ya mwaka 2022, matarajio yake binafsi, na shauku ya kurejesha heshima ya taifa…

Read More

Mzenji mikononi mwa Pamba Jiji

MABOSI wa Pamba Jiji wanasuka kikosi hicho kimyakimya ili kuongeza ushindani msimu ujao, ambapo wako katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa beki wa kati wa Singida Black Stars, Mukrim Issa ‘Miranda’ kwa mkopo. Nyota huyo kutoka Zanzibar msimu uliopita aliichezea Dodoma Jiji kwa mkopo pia akitokea Singida Black Stars, ambayo amebakisha nayo mkataba…

Read More

Ibenge aanza kuona mwanga Azam FC

KOCHA wa Azam FC, Florent Ibenge, ameonyesha imani na kuvutiwa na kiwango cha nyota wa timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Ibenge alitoa kauli hiyo baada ya timu hiyo kushinda mabao 4-0 dhidi ya Arusha Combine katika mchezo wa kirafiki…

Read More

Taifa Stars kanyaga twen’zetu robo

HAKUNA kitu kingine kinachosubiriwa na mashabiki wa soka nchini, ila kusikia na kuiona timu ya taifa, Taifa Stars ikivuka hatua ya makundi na kutinga robo fainali ya michuano ya Ubingwa wa Nchi za Afrika (CHAN) 2024 kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania. Stars inayoongoza msimamo wa Kundi B ikiwa pia ndio wenyeji wa…

Read More

Kwa hizi mbinu za Folz, mjipange!

UNALIKUMBUKA balaa la Miguel Gamondi alipokuwa Yanga kwa aina ya soka lake lilivyotingisha kabla ya kuondoka? Jamaa alipotoka tu, akaingia Sead Ramovic akafanya balaa ndani ya muda mfupi na ile ‘gusa achia twende kwao’ kisha akasepa. Mashabiki wa Yanga wakawa na presha baada ya kuondoka Ramovic, lakini akatua Miloud Hamdi na balaa la Gusa Achia…

Read More

Droo CAF…Wapinzani Yanga, Simba ni hawa

DROO ya michuano ya kimataifa kwa ngazi za klabu kwa msimu wa 2025-26 inafanyika leo mchana jijini Dar es Salaam, huku Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana na miongoni mwa timu 16 katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa mujibu wa muongozo wa droo hiyo ambao Mwanaspoti limeunasa kutoka kwa mmoja wa maofisa…

Read More