
Sikia alichosema beki mpya Yanga, awataja Bacca, Azizi KI
WAKATI Yanga ikiwa katika hatua za mwisho za kukamilisha mazungumzo kwa ajili ya kumsajili beki wa FC Lupopo, Chadrack Boka anayetakiwa kuja kuziba nafasi ya Lomalisa Mutambala, mwenyewe amefunguka kwamba: “Najua mashabiki wanachotaka, waambie wasubiri nakuja kuwafurahisha kwa kuipa timu kazi nzuri.” Boka ambaye ni mrefu kwa umbo, amefichua kwamba anasubiri uhamisho huo ukamilike haraka…