
Yanga kikitoka chuma, kinashuka chuma zaidi
Yanga wana msemo wao mmoja maridadi sana ‘Daima Mbele Nyuma Mwiko’, yaani hawana nafasi ya kujuta na wako tayari kuchukua maamuzi yoyote magumu na baada ya hapo hawaangalii nyuma. Msemo wao huu kuna namna umekuwa ukiwaheshimisha katika misimamo yao katika mambo mbalimbali ndani ya klabu yao na kama hujajua wanamaanisha nini, cheki haya mambo sita…