
Mandonga: Chakula cha buku hadi tv kila chumba
MEI 12, mwaka huu bondia wa ngumi za kulipwa nchini na mpiga debe wa zamani wa Kituo cha Mabasi Msamvu mjini Morogoro, Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ atakuwa akimaliza adhabu yake. Mandonga atamaliza adhabu hiyo iliyotokana na kusimamishwa kupanda ulingoni na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), kufuatia kupokea kipigo cha TKO ya raundi sita…