
JIWE LA SIKU: Simba ya Mgunda anakufunga yeyote
Simba imeanza maisha mapya baada ya kocha Abdelhak Benchikha kuondoka kwa ilichoelezwa kuwa ni matatizo ya kifamilia na timu kukabidhiwa kwa Juma Mgunda na Selemani Matola, uamuzi ambao kwa hakika umewapa matumaini makubwa mashabiki kutokana na rekodi za kocha huyo mzawa aliyejipatia sifa kama “mzee wa acha boli litembee.” Mgunda amerejea kikosini kama kaimu kocha…