Vituko vya wachezaji uwanjani | Mwanaspoti

Wakati mwingine wachezaji wanafanya vituko vya ajabu, hadi wao wenyewe wanajishangaa, pindi wanapopata utulivu wa kujitathimini baada ya majukumu yao, kuona walifanya vitu vya ajabu. Mwanaspoti limezungumza na wachezaji mbalimbali kujua wanakuwa wanapatwa na nini hadi wakati mwingine hufanya matukio ya kushangaza uwanjani na majibu yao yatakuchekesha na kukushangaza.  Beki wa Mashujaa, Said Makapu anasema…

Read More

Kocha Simba afikisha siku 526 rumande upelelezi bado!

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba, Muharami Sultani ‘Shilton’ (40) na wenzake wanaendelea kusota rumande kwa siku 526 sasa kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika. Sultani na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwemo ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89 pamoja na kutakatisha fedha. Kwa mara ya…

Read More

Robertinho: Simba inahitaji mambo mawili tu, itoboe!

SIMBA imeanza maisha mapya bila ya Abdelhak Benchikha aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo ikipata sare ya 2-2 na Namungo mjini Lindi katika Ligi Kuu Bara, huku kocha wa zamani wa klabu hiyo Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ akituliza upepo akisema kwa sasa inatakiwa kufanya mambo mawili tu hali iwe shwari. Simba imeachana na Benchikha aliyedumu…

Read More

Pamba yasimamisha Jiji, yapokelewa kishujaa Mwanza

Mwanza. USIPIME! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mapokezi makubwa iliyoyapata Pamba Jiji leo baada ya kupanda daraja kwenda Ligi Kuu Bara mwishoni mwa wiki iliyopita ikivunja mwiko wa miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001. Msafara wa timu hiyo uliokuwa umebeba wachezaji, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi uliokuwa unatokea Arusha kupitia mkoani Shinyanga…

Read More

Mtanda azikataa Simba, Yanga ndani ya Pamba

Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na mlezi wa timu ya Pamba Jiji, Said Mtanda amesema hatamvumilia mtu yeyote atakayeingiza U-Simba na U-Yanga ndani ya timu hiyo itakapokuwa inacheza mechi zake za Ligi Kuu Bara msimu ujao. Mtanda ametoa kauli hiyo leo Aprili 30, 2024 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa wakati akizungumza na maelfu…

Read More

Mgunda aanza na sare Simba

KAIMU Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda, ameanza majukumu yake ndani ya kikosi hicho kwa kuambulia sare katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC. Mchezo huo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa mkoani Lindi, umemalizika kwa sare ya mabao 2-2 ikiwa ni sare ya tatu mfululizo kwa timu hizo…

Read More

Sababu kwanini Mgunda anatosha Simba

Mashabiki wa Simba wamepata mzuka upya wakiwa na matumaini makubwa kwa kocha wa timu hiyo Juma Mgunda ambaye anasaidiana na Selemani Matola. Mgunda ambaye alikuwa timu ya Wanawake Simba Queens alirudishwa kwenye kikosi cha wakubwa baada ya kuondoka aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Abdelhak Benchikha juzi, kutokana na kile kinachodaiwa kuwa anasumbuliwa na matatizo…

Read More

Wazir Jr kinara wa ufungaji KMC FC ajiunga Meridianbet

    MUITE Wazir Jr ‘The King of CCM Kirumba’, kwa sasa anakipiga KMC FC inayodhaminiwa na kampuni namba moja kwa michezo ya ubashiri na kasino ya Mtandaoni– Meridianbet, wameungana na kufanya jambo kwa jamii anayoishi kijana huyu maeneo ya Kinyerezi-Tabata. Wazir Jr ikumbukwe kuwa ndiye mchezaji kinara wa upachikaji wa magoli kwa klabu ya…

Read More

Gamondi: Pacome atacheza | Mwanaspoti

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameibuka na kusema kiungo wake, Pacome Zouzoua yupo tayari kuanza kucheza na kesho Jumatano kuna uwezekano akampa nafasi, lakini itategemea na mazoezi ya mwisho leo jioni. Kauli ya Gamondi imekuja wakati kesho Yanga ikiwa na mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Tabora United utakaochezwa…

Read More

PUMZI YA MOTO: Mkasa wa Pamba FC kushuka daraja 2001

HATIMAYE Pamba ya Mwanza imefanikiwa kurudi Ligi Kuu Bara tangu ishuke daraja 2001. Klabu hiyo ambayo sasa inatambulika kama Pamba Jiji, imepanda baada ya ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Mbuni ya Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo. Pamba, klabu yenye rekodi yake barani Afrika inarudi Ligi Kuu baada ya kukaa chini…

Read More