
Yanga yagomea chumba cha kubadilishia nguo Kwa Mkapa
Muda mfupi baada ya Yanga kuwasili katika Uwanja wa Mkapa, wamelazimika kugomea kuingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Maofisa wa Yanga waliotangulia kukagua chumba hicho walionekana kutoridhishwa na mandhari waliyoyakuta ambapo walionekana kulalamika kuna hewa nzito na kuumia macho wakidai kutokwa machozi. Kutokana na ishu hiyo, wahusika wakuu wa mchezo huo akiwemo Mratibu Mkuu, Herieth Gilla, walifika…