
Dodoma Jiji, KMC vita ya nafasi Bara
LIGI Kuu Bara inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kupigwa ambapo Dodoma Jiji itakuwa kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kucheza na KMC. Dodoma ambayo huu utakuwa mchezo wake wa 23, ikishinda itasogea kutoka nafasi ya 10 iliyopo sasa na pointi 25 hadi ya nane na kuzishusha Namungo na Singida Fountain Gate zenye pointi 26…