
Gamondi, Benchikha wakutana na sapraizi Kwa Mkapa
Unaweza kusema ni kama makocha wa timu zote mbili, Miguel Gamondi wa Yanga na Abdelhak Benchikha wa Simba wamekutana na sapraizi, baada ya kulazimika kufanya mabadiliko ya mapema zaidi. Kwa kawaida, mabadiliko ya wachezaji kwenye mechi hufanyika kiufundi, lakini jana makocha hao walilazimika kuyafanya mapema bila ya kutarajiwa. Alianza Gamondi kufanya mabadiliko ya kumtoa Joyce…