Singida BS yamgeukia straika Mkongomani

BAADA ya Singida Black Stars kufikia makubalino na Simba ya kumuachia aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Mghana Jonathan Sowah, mabosi wa timu hiyo wako hatua nzuri ya kumpata mshambuliaji mpya raia wa DR Congo, Malanga Horso Mwaku. Sowah tangu ajiunge na kikosi hicho dirisha dogo la Januari 2025, akitokea Al-Nasr Benghazi ya Libya, alifunga mabao…

Read More

Mayele anukia Mtibwa Sugar | Mwanaspoti

MABINGWA wa zamani w Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar wanakaribia kuipata saini ya mshambuliaji wa TMA ya Arusha, Kassim Shaibu ‘Mayele’, baada ya nyota huyo kufanya mazungumzo na timu hiyo, ambayo hadi sasa yanaendelea vizuri ili kukitumikia kikosi hicho msimu ujao. Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata, zinaeleza Shaibu amekubaliana maslahi binafsi ya kujiunga na Mtibwa Sugar…

Read More

Mangalo apewa mwaka Pamba Jiji

BAADA ya kukaa nje ya uwanja kwa muda, beki wa zamani wa Biashara United na Singida Fountain Gate, Abdulmajid Mangalo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Pamba Jiji. Awali, beki huyo alikuwa anafanya mazungumzo na Mtibwa Sugar, lakini mambo hayakwenda vizuri sasa ni rasmi ataitumikia Pamba msimu ujao wa 2025-2026 unaoatarajiwa kuanza katikati ya Septemba….

Read More

Simba, Yanga kuanzia ‘mchangani’ CAF

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba na Yanga zimepangwa kwa pamoja kuanzia hatua ya awali ya raundi ya kwanza tofauti na misimu mitatu iliyopita zilipokuwa zikitofautiana kwa Simba kuanzia raundi ya pili. Hatu hiyo imetokana na mabadiliko yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa msimu ujao wa…

Read More

DR Congo yazinduka CHAN, yainyoa Zambia

BAADA ya kupoteza mechi ya kwanza ya mashindano ya CHAN 2024 inayoendelea kutimua vumbi ukanda wa Afrika Mashariki, DR Congo imepata ushindi wa kwanza jioni hii dhidi ya Zambia.  DR Congo ilianza michuano hiyo ilichapwa katika mechi ya kwanza dhidi ya wenyeji, Kenya ambao usiku huu wapo uwanjani kutupa karata ya pili katika michuano hiyo….

Read More

Kocha Simba apata chimbo Ghana

ALIYEKUWA kocha wa Simba Queens, Yussif Basigi ametambulishwa kwenye kikosi cha Police Ladies ya Ghana kuiongoza timu hiyo kwenye michuano ya WAFU kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake. Kocha huyo raia wa Ghana alihudumu Simba msimu mmoja akitokea Hasaacas Ladies ya nchini kwao, lakini hakufanikiwa kutetea ubingwa wa Ligi ya Wanawake akiushuhudia ukienda kwa…

Read More

Kisa Simba, maafande waitana kumjadili Yakoub

KIKAO kizito kinachotarajia kufanyika ndani ya wiki hii kati ya uongozi wa JKU Zanzibar na JKT Tanzania, kitahusu kinachoendelea kwa kipa Yakoub Suleiman kuhusishwa kutakiwa na Klabu ya Simba iliyopo jijini Ismailia, Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya. Mwanaspoti lina taarifa kutoka chanzo cha ndani kilichodai kwamba wachezaji askari wanapotoka Zanzibar kuja kucheza…

Read More

Mkenya kumchomoa mmoja Simba SC

BAADA ya Simba Queens kumrejesha mshambuliaji Mkenya Jentrix Shikangwa inaelezwa viongozi huenda wakavunja mkataba wa Magnifique Umutesiwase raia wa Rwanda. Hadi sasa Simba imesajili wachezaji sita wa kigeni ambao ni Zainah Nadende (Uganda), Ruth Aturo (Uganda), Zawadi Usanase (Rwanda), Cynthia Musungu (Kenya), Fasila Adhiambo (Kenya) na Magnifique Umutesiwase. Na wale waliokuwepo msimu uliopita ni Winifrida…

Read More