Pacome amuangukia Gamondi, kocha amgomea

SAA chache kabla ya Yanga kuanza safari ya kuja uwanjani kiungo wa timu hiyo amewasilisha maombi kwa kocha wake ampe hata dakika 20 za mchezo huo. Taarifa kutoka ndani ya Kambi ya Yanga ni kwamba baada ya kiungo huyo kufanya mazoezi vizuri ya siku tatu na kikosi hicho, akawasilisha maombi hayo kwa Gamondi, lakini akagoma….

Read More

Saa 4 kabla ya mechi, Kwa Mkapa jua kaliii

Zikiwa zimesalia takribani saa nne ili kuchezwa kwa mechi ya Watani wa Jadi Yanga dhidi ya Simba, hali ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, imepoa. Wakati saa zikizidi kusogea na jua likiwa kali katika maeneo ya uwanja, mpaka sasa hali bado si ya kuridhisha kwa upande wa mashabiki. Rangi zinazoonekana kwa wingi maeneo haya ni kijani…

Read More

Kakolanya aigomea Singida | Mwanaspoti

SIKU chache baada ya Kamati ya Nidhamu ya Singida Fountaine Gate kumuandikia barua kipa wao, Beno Kakolanya kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili za kutoroka kambini na kuihujumu timu, staa huyo ameitikia wito huo, lakini amekataa kuhudhuria kikao. Kwa mujibu wa Singida Fountaine Gate, Kakolanya amejibu barua ya wito kuwa hataweza kufika kwenye kikao cha…

Read More

Yanga kutembea na upepo wa Arajiga leo?

YANGA inashuka kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni kupambana na watani zao, Simba, huku timu hiyo ikiwa na rekodi bora msimu huu wakati michezo yao ya Ligi Kuu Bara ilipochezeshwa na mwamuzi wa kati, Ahmed Arajiga. Arajiga kutokea mkoani Manyara ndiye aliyepewa jukumu la kutafsiri sheria 17 za soka baina ya timu hizo, huku…

Read More

Usalama waimarishwa Kwa Mkapa | Mwanaspoti

LICHA ya uchache wa mashabiki kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Yanga dhidi ya Simba unaotarajiwa kupigwa saa 11:00 jioni, usalama umeimarishwa kila kona. Kama Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam lilivyoahidi ulinzi kufanyika barabara zote zilizo karibu na Uwanja wa Mkapa, hilo limefanyika kwani wamejazwa kila kona. Ili kuhakikisha usalama…

Read More

Vita ya mabingwa wa CAF yaanza upya!

Achana na Kariakoo Dabi itakayopigwa kuanzia saa 11:00 jioni kwa vigogo Simba na Yanga kuvaana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, saa moja kabla huko Lubumbashi, DR Congo kutakuwa na vita ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji TP Mazembe dhidi ya watetezi Al Ahly ya Misri. Baada ya pambano hilo la…

Read More

Neema ya Kariakoo Dabi kiuchumi

Achana na burudani wanayopata mashabiki wa soka nchini inapokuja Dabi ya Kariakoo, lakini ukweli, pambano hilo la watani wa jadi nchini, limekuwa na neema kubwa kwa wachuuzi na wafanyabiashara waliopo kando ya Uwanja wa Benjamin Mkapa na maeneo ya jirani. Wakati leo pambano hilo likitarajiwa kupigwa kuanzia saa 11:00 jioni tayari wafanyabiashara wadogo wadogo na…

Read More

Jumamosi yaibeba Yanga Kariakoo Dabi

MASHABIKI wa Yanga na Simba tayari viroho vimeanza kuwadunda, wakati wakiendelea kuhesabu siku kabla ya timu zao kushuka katika pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa Jumamosi hii ya Aprili 20, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Kitendawili cha nani mbabe kitateguliwa Jumamosi hii ingawa Yanga inaingia katika mchezo huo ikiwa na morali…

Read More

Singida FG, Mashujaa vita ya matumaini

KESHO Jumapili Singida Fountain Gate na Mashujaa FC zitakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu za matumaini ya kubaki Ligi Kuu Bara na kumaliza nafasi za juu kwenye msimamo zitakapokutana katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuanzia saa 10:00 jioni. Kocha Msaidizi wa Mashujaa FC, Makatta Maulid (kushoto) na mchezaji wa timu hiyo Shadrack Ntabindi wakizungumzia…

Read More