Matola: Yanga ni bora ila msikariri!

KOCHA Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema hakuna mechi rahisi ya dabi wanawaheshimu wapinzani wao kutokana na kuwa bora lakini wao pia wamejiandaa kukabiliana nao. Matola amesema mchezo wa kesho ni mchezo tofauti na uliopita pamoja na ubora wa Yanga na wao wamejiandaa kuhakikisha wanapata matokeo. ”Hii ni mechi mpya na kutakuwa na mbinu tofauti,…

Read More

10 za Kariakoo Dabi si mchezo!

JUMAMOSI ya wiki hii, kuna Kariakoo Dabi inapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ni wenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara wakiikaribisha Simba. Hii ni Kariakoo Dabi ya 112 ndani ya Ligi Kuu, huku tukiwa na kumbukumbu ya ile ya mzunguko wa kwanza, waliokuwa wageni, Yanga waliibuka na ushindi mnono wa…

Read More

Simba kujichimbia hoteli ya kifahari

SIMBA inatarajia kutua jijini Dar es Salaam leo alasiri, ikitokea Zanzibar ambako iliweka kambi ya siku tatu, kujiandaa na Kariakoo Dabi dhidi ya mtani wake Yanga, itakayopigwa kesho kuanzia saa 11:00 jioni, Uwanja wa Benjamin Mkapa. Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, zinasema hadi kufikia saa tisa alasiri, watakuwa wamefika mjini na wataweka…

Read More

Dabi ya Aziz KI na Chama

UKISIKIA mwisho wa ubishi ndio huu wakati vigogo vya soka nchini, Simba na Yanga zitavaana katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara. Ndio, kesho kuna Dabi ya Kariakoo itakayopigwa kuanzia saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam huku kila mmoja ikiwa na kumbukumbu ya mechi iliyopita iliyopigwa Novemba 5…

Read More

Mechi inayofuata baada ya kipigo kikubwa -3

TUNAENDELEA na simulizi zetu za mechi ijayo ya watani wa jadi, Aprili 20 mwaka huu…yaani Jumamosi hii! Hii ni mechi ya kwanza tangu Yanga wawape watani wao Simba kipigo kikubwa cha 5-1, Novemba 5, 2023. Hiki ni moja ya vipigo vikubwa ambavyo vimewahi kutokea kwenye mechi watani. Kupitia makala hizi tunakuletea kumbukumbu ya mechi iliyofuata…

Read More

Vita iko hapa Kariakoo Dabi

MECHI za watani wa jadi huweza kuamuliwa na uwezo binafsi wa washambuliaji, viungo na mara chache mabeki, lakini mbinu za kocha zinaweza pia kuwa nguzo ya timu kupata matokeo iliyokusudia. Mara kadhaa ustadi binafsi wa wachezaji kama Emmanuel Okwi, Dua Said, Omary Hussein ‘Keegan’, Abeid Mziba ‘Tekero’, Abdallah Kibadeni ‘King Mputa’, Amissi Tambwe, Mohamed Hussein…

Read More

Benchikha na msala wa 5-1 za Yanga SC

Ilikuwa Novemba 5, 2023 uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Yanga iliichapa Simba mabao 5-1 kwenye mechi ya ligi na kupelekea kufutwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu wa wekundu wa Msimbazi, Roberto Oliveira ‘Robertinho’. Ni mechi iliyokuwa na hisia mbili tofauti. Furaha kwa wageni Yanga. Huzuni kwa kwa wenyeji Simba. Iliichukua Yanga dakika tatu kuandika bao…

Read More

NIONAVYO: Kombe la Dunia la klabu ni vita mpya ya pesa

TANZANIA, Afrika Kusini na labda Afrika nzima mitandao imejaa mjadala wa uamuzi wa kutia shaka wa refa wa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliozikutanisha Young Africans au Yanga na Mamelodi Sundowns au Masandawana ya Pretoria, Afrika Kusini. Kutolewa kwa Yanga ni kilio kwa wapenzi wa Yanga, lakini ni kicheko kwa watunzaji…

Read More