
NJE YA BOKSI: Mapambano haya yaliwaletea neema
NEVADA, MAREKANI: Kazi kazi. Mchezo wa ngumi ni moja ya michezo inayolipa pesa ndefu kwa mabondia kupanda ulingoni. Haijalishi bondia atapigana kwa muda gani. Wapo wanaopanda na kushuka kwa maana ndani ya sekunde chache tu wameshakalishwa, lakini hilo haliwazuiii kuchota chao. Malipo kama kawa. Ni moja ya michezo ambayo uhakika wa pesa ni nje nje….