Straika Kagera atimkia Kenya | Mwanaspoti

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Kagera Sugar raia wa Cameroon, Moubarack Amza amekamilisha usajili wa kujiunga na Bandari FC ya Kenya, itakayocheza mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Yanga katika kilele cha ‘Wiki ya Mwananchi’ Septemba 12. Nyota huyo atacheza dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, katika tamasha la kikosi hicho…

Read More

Adam apigia hesabu mpya Tabora United

MSHAMBULIAJI wa Tabora United, Adam Adam amesema mashindano ya Tanzanite Pre-Season International Tournament yaliyoandaliwa na Fountain Gate na kufanyika kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara, yanawasaidia kuwaweka tayari kimwili na kimbinu kwa ajili ya hesabu mpya za msimu wa Ligi Kuu Bara inayotarajia kuanza Septemba 17. Nyota huyo wa zamani wa Azam, Tanzania…

Read More

Gamondi amtaja Tchakei, suluhu ya Wahabeshi

BAADA ya kuambulia pointi moja kupitia suluhu ya mechi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Kagame 2025, kocha Miguel Gamondi amesema walikosa mchezaji mbunifu wa kufungua ukuta wa wapinzani wao, Coffee ya Ethiopia huku akimtaja Marouf Tchakei. Singida ilipata suluhu ya mechi za Kundi A ya michuano hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali…

Read More

Tabora United yasaka kipa, Chilunda ndani

UONGOZI wa Tabora United umeingia sokoni kusaka kipya mpya baada ya tegemeo namba moja, Fikirini Bakari, kuvunjika taya katika mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga iliyowafunga mabao 4-0 katika Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam. Chanzo cha Mwanaspoti kimesema Bakari aliyemaliza akiwa na ‘clean sheet’ moja aliyoipata akiwa Fountain Gate kabla ya kujiunga wakati dirisha…

Read More

Wanne waliofunika robo fainali Ligi ya Kikapu Dar

WACHEZAJI wanne kutoka JKT, Dar City, Tausi Royals na DB Troncatti walikuwa kivutio katika robo fainali ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kutokana na kuwa na uwezo mzuri wa kucheza na kuchezesha timu katika nafasi zao, mambo ambayo yalizibeba na kuziwezesha kushinda. Wachezaji hao Omary Sadick (JKT), Amin Mkosa (Dar City),…

Read More

Ndayiragije azitamani poini tatu za Singida BS

POLISI Kenya imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Kagame 2025 kwa kuifumua Garde Cotes ya Djibouti kwa mabao 4-0, lakini kocha mkuu wa timu hiyo, Etienne Ndayiragije amesema kwa sasa hesabu zake amezielekeza kesho Ijumaa watakapoikabili Singida Black Stars ya Tanzania. Mabingwa hao wa Kenya ambao watakashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, walianza kwa kishindo…

Read More

Nangu, Yakoub wapata warithi jeshini

BAADA ya JKT Tanzania kutangaza kuachana na kipa Yakoub Suleiman na beki Wilson Nangu waliojiunga na Simba, kocha wa timu hiyo, Ahmad Ally amesema ameshapata mbadala wao. Nangu na Yakoub wamesajiliwa Simba kila mmoja akisaini mkataba wa miaka mitatu, jambo ambalo Ally limemfurahisha akiona kwamba vijana wake wamewapa heshima kubwa JKT Tanzania. Alisema katika nafasi…

Read More

Mtumbuka: Ni muda wa kung’ara Tanzania Prisons

BAADA ya kushindwa kung’ara msimu uliopita akiwa na kikosi cha Mashujaa, winga Emmanuel Mtumbuka amesema ni wakati wa kufanya vizuri na kuonyesha uwezo wake baada ya kutimkia Tanzania Prisons ya Mbeya. Mtumbuka aliyedumu Mashujaa kwa mwaka mmoja baada ya kujiunga nayo msimu uliopita akitokea Stand United ya Shinyanga, alishindwa kupata uhakika wa namba na sasa…

Read More

Gamondi autaka ubingwa Cecafa Kagame Cup

KOCHA wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi ametangaza kuwa lengo kubwa kwenye michuano ya Cecafa Kagame Cup 2025 ni kuipa timu yake ubingwa akiitumia pia kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya kimataifa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara. Gamondi, aliyewahi kuinoa Yanga, ameanza jana, Jumanne safari yake na Singida kwenye mchezo wa Kundi…

Read More