Kocha mpya Yanga ashuhudia mavitu ya Mzize Stars

KOCHA mpya wa Yanga, Romain Folz ni miongoni mwa watu waliofika katika Uwanja wa Mkapa kushuhudia mchezo wa ufunguzi kati ya Tanzania na Burkina Faso katika ufunguzi wa mashindano ya CHAN. Kocha huyo ameambatana na benchi lote la wasaidizi wake ambao ni kocha wa makipa, mkurugenzi wa benchi la ufundi na kocha wa viungo wote…

Read More

Rayvanny aibua shangwe ufunguzi CHAN 2024

DAKIKA chache kabla ya mchezo wa ufunguzi kati ya wenyeji Tanzania dhidi ya Burkina Faso uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rayvanny ameibua shangwe kwa mashabiki. Staa huyo ameingia uwanjani kutumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo akiimba wimbo wa Kitu Kizito aliomshirikisha Misso Misondo na kuibua vaibu kubwa…

Read More

Morocco ataja jeshi la kuivaa Burkina Faso, Mzize aachiwa msala

KOCHA wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, ametaja kikosi cha nyota 11 watakaoanza katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya CHAN 2024 dhidi ya Burkina Faso. Katika kikosi hicho, Clement Mzize atakuwa anaongoza mashambulizi, akishirikiana na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na Iddi Seleman ‘Nado’ watakaotokea pembeni huku Feisal Salum ‘Fei Toto’ akiunganisha safu ya kiungo cha…

Read More

Stars kusaka rekodi mpya CHAN 2024

WAKATI ikibakia saa chache kabla ya kushuhudia mechi ya ufunguzi wa michuano ya Fainali za Ubingwa kwa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 kati ya wenyeji timu ya taifa ya Tanzania maarufu Taifa Stars dhidi ya Burkina Faso, kikosi cha Stars kinaingia kusaka rekodi mpya kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Rekodi ambayo…

Read More

Azam FC, Yanga zaingia vitani

INAELEZWA kwamba uongozi wa Azam na Yanga umeingia katika vita nzito baada tu ya usajili wa beki ambaye pia ana uwezo wa kucheza kiungo mkabaji, Abubakar Nizar Othman ‘Ninju’, aliyesajiliwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2024-2025 akitokea JKU SC ya Zanzibar. Ninju ametangazwa rasmi kujiunga na Yanga ambapo usajili wake…

Read More

Kwa Mkapa usalama freshi, mashabiki mdogomdogo

LICHA ya kutokuwa na vaibu kubwa la mashabiki kwa sasa, lakini hali ya usalama kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa utakaotumika kwa pambano la ufunguzi wa michuano ya CHAN kati ya Taifa Stars na Burkina Faso ni ya aina yake kutokana na polisi kuwa kila kona kuhakikisha hakutokei kihatarishi cha usalama. Leo, Agosti 2, 2025 Tanzania…

Read More

Dah! Kwa Mkapa bado | Mwanaspoti

Muonekano wa mashabiki katika Uwanja wa Benjamin Mkapa siyo kama vile ambavyo ulitarajiwa kutokana na nyomi ya ilivyokuwa nje ya uwanja mapema leo kabla ya kuruhusiwa kuanza kuingia. Kabla ya mageti kufunguliwa watu walijaa nje ya uwanja wakisubiri kuingia ili kushuhudia mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Burkina Faso inayotarajiwa kuchezwa saa 2:00 usiku,…

Read More

18 wapenya usaili RT,  Ikangaa, Isangi wajiondoa

Kuelekea uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), unaotarajiwa kufanyika Agosti 16 mwaka huu jijini Mwanza, wagombea 18 wamefaulu katika mchujo wa awali. Mchakato huo umetawaliwa na matukio ya kushtua ikiwemo kujiondoa kwa nyota wa zamani wa riadha nchini, Juma Ikangaa  pamoja na rais aliyemaliza muda wake, Silas Isangi ambao walitangaza uamuzi huo wakiwa…

Read More

Kwa Mkapa kila kitu shwari

UTARATIBU wa kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa unaotarajiwa kupigwa mechi ya ufunguzi wa michuano ya Chan kati ya Tanzania na Burki Faso umezingatia ustaarabu. Kabla ya mageti kufunguliwa nyomi ya watu ilijaa nje ya uwanja, wakisubiri kuingia ili kushuhudia mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kuanzia saa 2:00 usiku, lakini baada ya kuruhusiwa kila kitu kinakwenda bila…

Read More

CHAN yabadili utaratibu kwa Mkapa

TOFAUTI na ilivyozoeleka katika mechi nyingi za ndani, ambapo mageti ya viwanja hufunguliwa mapema ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuingia mapema, hali imekuwa tofauti kwenye ufunguzi wa mashindano ya CHAN 2024. Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao utatumika kwa ufunguzi wa mashindano hayo ulinzi ni mkubwa  huku mashabiki wakizuiwa kuingia mapema kama ilivyo kawaida. Mashindano hayo…

Read More