Diarra dhidi ya Lakred | Mwanaspoti

WAKATI homa ya pambano la Ligi Kuu Bara kati ya vinara wa ligi, Yanga dhidi ya Simba likizidi kupanda kutakuwa na vita nyingine mpya kwenye eneo la makipa wa timu hizo mbili. Hapana shaka Yanga golini nafasi kubwa itakuwa kwa kipa namba moja, Djigui Diarra ambaye sio mgeni wa mechi hizo akicheza mechi yake ya…

Read More

Kapombe aipiga mkwara mzito Yanga

Beki mkongwe wa Simba, Shomari Kapombe amesema watatumia mchezo wa kesho kurudisha matumaini ya kutwaa taji msimu huu huku akikiri wananafasi kubwa ya kufanya hivyo. Kapombe amesema benchi la ufundi limefanyia kazi maeneo yote lakini matatu ndio yalifanyiwa kazi kwa usahihi zaidi lengo likiwa ni kufikia malengo yao. “Kocha ameangalia makosa kwenye mechi zilizopita amehakikisha…

Read More

Matola: Yanga ni bora ila msikariri!

KOCHA Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola amesema hakuna mechi rahisi ya dabi wanawaheshimu wapinzani wao kutokana na kuwa bora lakini wao pia wamejiandaa kukabiliana nao. Matola amesema mchezo wa kesho ni mchezo tofauti na uliopita pamoja na ubora wa Yanga na wao wamejiandaa kuhakikisha wanapata matokeo. ”Hii ni mechi mpya na kutakuwa na mbinu tofauti,…

Read More

10 za Kariakoo Dabi si mchezo!

JUMAMOSI ya wiki hii, kuna Kariakoo Dabi inapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ni wenyeji wa mchezo huo wa Ligi Kuu Bara wakiikaribisha Simba. Hii ni Kariakoo Dabi ya 112 ndani ya Ligi Kuu, huku tukiwa na kumbukumbu ya ile ya mzunguko wa kwanza, waliokuwa wageni, Yanga waliibuka na ushindi mnono wa…

Read More

Simba kujichimbia hoteli ya kifahari

SIMBA inatarajia kutua jijini Dar es Salaam leo alasiri, ikitokea Zanzibar ambako iliweka kambi ya siku tatu, kujiandaa na Kariakoo Dabi dhidi ya mtani wake Yanga, itakayopigwa kesho kuanzia saa 11:00 jioni, Uwanja wa Benjamin Mkapa. Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, zinasema hadi kufikia saa tisa alasiri, watakuwa wamefika mjini na wataweka…

Read More

Dabi ya Aziz KI na Chama

UKISIKIA mwisho wa ubishi ndio huu wakati vigogo vya soka nchini, Simba na Yanga zitavaana katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Bara. Ndio, kesho kuna Dabi ya Kariakoo itakayopigwa kuanzia saa 11:00 jioni kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam huku kila mmoja ikiwa na kumbukumbu ya mechi iliyopita iliyopigwa Novemba 5…

Read More