Tuzo za wanamichezo bora BMT zaiva
WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limeandaa tuzo za wanamichezo bora mwaka 2023 zinazotarajiwa kufanyika Juni 9, 2024 kwenye Ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki, Dar es Salaam. Tuzo hizo ni mara ya pili kufanyika baada ya mwaka jana, Machi 17, 2023 kwenye Ukumbi wa Mlimani City. Mwenyekiti wa BMT,…