
Bado Watatu – 17
“HEBU eleza tukio lilivyotokea.” Akaniambia kwamba yeye alikuwa muuguzi wa hospitali ya Bombo ambayo ni ya mkoa. Jana yake alikuwa na zamu ya kulala kazini. Lakini aliporudi asubuhi kutoka kazini akakuta wezi wameruka ukuta na kuvunja mlango wa nyuma na kumuibia vitu kadhaa. “Unasema waliruka ukuta wakavunja mlango wa nyuma?” “Ndiyo.” “Wameiba nini?” “Labda niseme…