Yanga yashtukia mtego, Gamondi aita kikao na mastaa

MASHABIKI wameshaanza kushona jezi za Ubingwa wa Yanga msimu huu, lakini Kocha Miguel Gamondi ameshtukia mechi mbili zinazofuata zina mtego mkubwa kwao na akawaweka chini wachezaji wake. Gamondi ameliambia Mwanaspoti amewasisitiza wachezaji wake wasijisahau kwani wanakwenda kucheza na timu ambazo zimechukua tahadhari kubwa kuliko kawaida na zina malengo mengi. Kocha huyo amesisitiza anaamini kila mchezaji…

Read More

Staa Asec aomba kusepa, atajwa kutua Simba

KIUNGO mshambuliaji wa Asec Mimosas, Serge Pokou ameomba rasmi kuondoka klabuni hapo huku akihusishwa na Simba inayoelezwa inampigia hesabu kali. Fundi huyo wa mguu wa kushoto ambaye aliwahi kuifunga Simba hapa nchini wakati timu hizo zilipokutana Ligi ya Mabingwa alisema ingawa ana ofa nyingi lakini amevutiwa na ofa ya Tanzania. “Nina ofa nyingi ikiwemo moja…

Read More

CITY BULLS, JKT PAMOTO DAR KESHO

UWANJA wa kikapu wa DB Osterbay unatarajiwa kuwaka moto wakati timu kongwe za kikapu nchini, JKT na Vijana (City Bulls) zitakapochuana kesho katika mchezo wa Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL). Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na wapenzi wa kikapu mkoani humo kutokana na upinzani mkubwa zilio nao timu hizo.  Timu…

Read More

Thiago Silva kama kawa amemalizia hisani nyumbani

YUKO wapi yule aliyesema hisani inaanzia nyumbani? Wazungu huwa wanaandika kwa Kiingereza chao kizuri ‘charity begins at home’. Ni kweli. Lakini Wabrazil nao wangeweza kuendeleza sentensi hiyo na kuandika ‘hisani pia inaishia nyumbani’. Wiki ile nyingine nilimuona Mbrazili Thiago akilia katika viunga vya uwanja wa mazoezi wa Chelsea, Cobham. Labda ana hisia kali na Chelsea…

Read More

Sababu sita Mgunda apewe timu, wakongwe wafunguka

FURAHA imerejea Simba. Mabadiliko yaliyofanywa kwenye benchi la ufundi na kumrejesha Juma Mgunda yameanza kulipa. Ametumia mechi nne tu kubadilisha mambo ndani ya klabu na sasa imefikia hatua wakongwe wamesema apewe timu. Si hao tu, hata mashabiki baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam juzi na kufufua matumaini ya kushiriki Ligi ya Mabingwa…

Read More

Stand United, Copco tiketi iko Kambarage

 Mwanza. BAADA ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United, Copco imesema inaenda kumaliza dakika 90 za marudiano ikihitaji sare au ushindi ili kujihakikishia kubaki salama kwenye Championship msimu ujao. Timu hiyo ikicheza nyumbani kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza iliishindilia Stand United mabao 2-0 katika mchezo wa mchujo (play off) hatua ya kwanza na…

Read More

Mudathir afichua siri mabao ya jiooooni

KUNA siri kubwa nyuma ya mabao anayofunga kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya ambayo itawafunza wachezaji wengine kuzingatia baadhi ya mambo wanayoambiwa na makocha. Mwanaspoti limebaini kwamba asilimia kubwa ya mabao yake (tisa) amefunga kipindi cha pili, machache akifunga kile cha kwanza na Mudathri amefichua siri iliyopo. Sababu aliyoitaja Mudathir wanaporudi vyumbani, kitu kikubwa ni kusikiliza kwa…

Read More

Haya ndio maajabu ya beki anayetajwa kutua Yanga

BEKI anayetajwa kusajiliwa Yanga, Chadrack Boka kutoka FC Lupopo ya DR Congo, inaelezwa anapokuwa uwanjani ni mmyumbulikaji katika kufanya majukumu zaidi ya nafasi yake na pia ana kasi na nguvu. Shuhuda wa hilo ni beki wa Lubumbashi Sport ya DR Congo, Mtanzania Abdallah Shaibu ‘Ninja’ aliyesema baada ya kukutana naye kwenye mechi ya ligi kuu,…

Read More

Mgunda alivyowaficha mastaa wa Azam FC

UWEPO wa Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin katika eneo la kiungo cha Simba kuiwapa wakati mgumu Azam FC ambayo ilikumbana na kipigo cha mabao 3-0 jana, Alhamisi, katika mchezo wa vita ya kuwania kumaliza msimu kwenye nafasi mbili za juu katika Ligi Kuu Bara. Kabla ya mchezo huo ambao ulichezwa kwenye Uwanja wa…

Read More