Mechi tisa za Mgunda kutembeza boli hizi hapa

JUMA Mgunda na Seleman Matola wanaanza kibarua chao ndani ya Simba Jioni hii. Lakini ana mechi tisa mkononi ambazo atalazimika kutembeza boli kwa namna yoyote ile kutetea hadhi ya Simba kwenye Ligi Kuu Bara. Matokeo ya mechi hizo ndiyo yaliyobeba hatma ya Simba msimu ujao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwani ili washiriki lazima wabaki…

Read More

Mabao yatawabakisha Ligi Kuu | Mwanaspoti

MSIMU wa Ligi Kuu 2023/2024 unakaribia ukingoni na timu pamoja na wachezaji wanakaribia kuvuna kile walichokipanda ambacho ni ama kumaliza vizuri au kumaliza vibaya pindi mizunguko 30 ya ligi itakapokamilika. Timu mbili ambazo zitamaliza zikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi zitashuka daraja moja kwa moja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 13 na 14 zitacheza mechi…

Read More

Serikali kuunda timu tatu kuelekea Afcon 2027

Dodoma. Serikali ina mpango wa kuunda timu tatu imara za soka za Taifa kulingana na umri ambazo zitashiriki mashindano ya Afcon 2027 na mengine ambayo nchi itashiriki. Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma amesema hayo leo Jumatatu Aprili 30, 2024 alipojibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mwanakhamis Kassim…

Read More

Samasoti baharini inayolipa vijana mkwanja wa maana

MAKACHU ni mchezo unaochezwa sana maeneo ya Forodhani, Zanzibar katika Bahari ya Hindi, kwa wachezaji kujirusha umbali mrefu kutoka nchi kavu hadi majini. Lakini, nyuma ya mchezo huo kuna makanja wa maana tu ambao wanaingiza vijana wanaocheza makachu, kwani kwa wastani kila siku huingiza takriban Sh50,000 ambapo kwa mwezi ni zaidi ya Sh1.5 milioni. Kwa…

Read More

PUMZI YA MOTO: Mkasa wa Pamba FC kushuka daraja 202

HATIMAYE Pamba ya Mwanza imefanikiwa kurudi Ligi Kuu Bara tangu ishuke daraja 2001. Klabu hiyo ambayo sasa inatambulika kama Pamba Jiji, imepanda baada ya ushindi mnono wa 3-1 dhidi ya Mbuni ya Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini humo. Pamba, klabu yenye rekodi yake barani Afrika inarudi Ligi Kuu baada ya kukaa chini…

Read More

Che Malone, Inonga yawakuta Simba

Kwa namna Simba ilivyokuwa rahisi kuruhusu mabao msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, beki wa zamani wa timu hiyo, Boniface Pawasa amesema msimu ujao lazima uamuzi mgumu ufanyike wa kusajili beki mwingine mwenye uwezo wa kuituliza safu hiyo ya ulinzi kwa maana, waliopo wameshindwa kutimiza majukumu yao. Pawasa ambaye alifanya makubwa ndani ya timu…

Read More

Msala wa kwanza wa Mgunda Ligi Kuu

Siku moja baada ya kuachana na kocha wake Abdelhak Benchikha Simba inarudi uwanja  kwenye uwanja mgumu ugenini itakapokutana na wabishi Namungo ya Lindi. Simba baada ya kuondokewa na Benchikha aliyerusha taulo kwa sababu za kifamilia akiachana na timu hiyo, leo kikosi chao kitakuwa chini ya kocha wa Juma Mgunda ambaye atasaidiana na Seleman Matola. Matola…

Read More

Kuondoka kwa makocha Simba… Tatizo lipo hapa

LICHA ya Simba kutajwa timu yenye mafanikio kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na rekodi nzuri kimataifa ikiwa namba tano kwa ubora Afrika ndio timu pekee ambayo imefundishwa na makocha tisa ndani ya misimu sita. Simba imeandika rekodi hiyo ya kuachana na makocha hao baada ya juzi kuachana na Abdelhak Benchikha ambaye amedumu kwenye kikosi…

Read More

Aussems: Tatizo Simba ni lilelile

BAADA ya Abdelhak Bechikha kuachana na Simba kwa kile kilichotajwa ana matatizo ya kifamilia, kocha wa zamani wa timu hiyo, Patrick Aussems amesema tatizo la Simba ni lile lile. Aussems aliyeinoa Simba kuanzia Julai 2018 hadi Novemba 2019 amesema tatizo la Simba kutodumu na makocha wengi ni viongozi kutokuwa waadilifu jambo ambalo alilolisema wakati anaondoka….

Read More