USM Alger yagoma kuingiza timu uwanjani
Bingwa mtetezi wa Kombe la Shirikisho Afrika, USM Alger ya Algeria imegoma kuingiza timu kwenye Uwanja wa Berkane Municipal kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo dhidi ya RS Berkane ya Morocco, uliopangwa kupigwa saa 4:00 usiku. USM Alger ilifika hadi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo lakini hawakuingia uwanjani na…