Hii ndiyo Simba ya Sowah

BAADA ya msimu wa 2024/25 kukamilika patupu kwa Simba bila kutwaa taji lolote kubwa ndani na nje ya nchi, macho yote yakageuka kwa benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Fadlu Davids kuona hatua gani inafuata katika mradi wake. Kocha huyo kijana raia wa Afrika Kusini hakulaza damu. Alichora ramani ya namna ambavyo…

Read More

Simba yatua tena Mamelodi ikitaka winga

SIMBA haipoi. Baada ya kudaiwa kunasa saini ya mmoja wa mabeki wa Mamelodi Sundowns, mara hii imerejea tena ikipambana kuchomoa mtu ndani ya timu hiyo ambaye katika mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu kule Marekani ulimshuhudia akikipiga katika kikosi hicho. Achana na Rushine De Reuck, beki unayeweza kumuona mitaa ya Msimbazi msimu ujao, lakini…

Read More

Sifa nne beki mpya Simba

WAKATI mashabiki wa Simba SC wakifurahia taarifa za usajili wa beki wa kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck, mmoja wa wapinzani wake wa muda mrefu katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Qobolwakhe Sibande, ametia neno kuhusu ubora wake huku akitaja mambo manne aliyonayo. Sibande anayekipiga klabu ya TS Galaxy, aliwahi kukutana na De Reuck…

Read More

EAGT Temeke kuongoza maombi ya kitaifa kuombea uchaguzi mkuu

Dar es Salaam. Wakati taifa linapoelekea katika kipindi cha uchaguzi, waumini wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Temeke kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kiroho wameandaa mkutano wa injili ukiwa na lengo la kuwaombea Watanzania amani, mshikamano, na uongozi wenye maadili kuelekea uchaguzi ujao. Maombi hayo yanatarajiwa kuanza kesho Julai 27, 2025…

Read More

Mrithi wa Shomary huyu hapa!

UONGOZI wa KMC FC, uko katika mazungumzo ya kuipata saini ya beki wa kushoto wa kikosi cha Tanzania Prisons, Samson Mwaituka, kwa lengo la kuchukua nafasi ya Rahim Shomary aliyejiunga na Ghazl El Mahalla ya Misri. Samson alionyesha uwezo mkubwa na timu hiyo ya maafande kwa msimu wa 2024-2025, baada ya kuaminiwa kikosi cha kwanza…

Read More

Vipaji vya mastaa Bara nje ya soka

NYAKATI za sayansi na teknolojia kama mtu anataka kipaji chake kiende mbali anahitaji ubunifu na kujua mashabiki wake wanahitaji kitu gani. Ndivyo ilivyo kwa baadhi ya wanasoka wanaoweza wakapata mamilioni nje ya kazi hiyo. Kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, TikTok, Facebook na mingineyo inaweza ikawatoa kwa kuziposti kazi zao ilimradi zipendwe na kupokewa na…

Read More

Ramovic achomoa mtu Yanga | Mwanaspoti

Pale Yanga kuna watu wa maana kabisa, kwani kila kocha aliyeifundisha timu hiyo misimu ya karibuni na kuondoka, amesepa akiwa na vichwa ambavyo kokote atakakokwenda anatamani kupiga navyo kazi. Alianza Nasrredine Nabi aliyepo Kaizer Chiefs kwa sasa, Miguel Gamondi yupo Singida Black Stars aliyefuatiwa na Sead Ramovic anayeinoa CR Belouizdad kisha Miloud Hamdi aliyepo Ismailia…

Read More

Kigogo Prisons afichua mtoko mpya

“PRISONS mpya inakuja.” Ni kauli ya ofisa mtendaji mpya wa Tanzania Prisons, Godfrey Madegwa akieleza namna anavyokwenda kuisuka timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao, huku akiwatoa hofu wadau na mashabiki juu ya presha iliyojitokeza msimu uliopita. Msimu uliopita maafande hao waliponea chupuchupu kushuka Ligi Kuu Bara kufuatia matokeo ya jumla ya mtoano baada ya…

Read More

Manyama kuibukia Mtibwa | Mwanaspoti

BAADA ya kumalizana na Singida Black Stars, Edward Charles anatajwa kujiunga na Mtibwa Sugar iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu. Manyama ambaye alishawahi kukipiga Azam FC aliitumikia Singida Black Stars kwa mkataba wa mwaka mmoja na alijiunga nayo akitokea Azam FC aliyoitumikia kwa misimu miwili. Chanzo cha kuaminika kutoka Mtibwa Sugar kimeliambia Mwanaspoti kuwa mazungumzo…

Read More

Mwijage azikwepa mbili na kutua KMC

BAADA ya kuhusishwa na Pamba Jiji na Mtibwa Sugar aliyekuwa winga wa Kagera Sugar iliyoshuka Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Erick Mwijage amejiunga na KMC. Winga huyo ambaye alikuwa anahusishwa kujiunga na Pamba Jiji na Mtibwa Sugar amefikia makubaliano ya kusaini mkataba wa kuitumikia KMC kwa mkataba wa miaka miwili. Mwanaspoti limethibitishiwa na mmoja ya…

Read More