Wananchi Dar walia bili kubwa za maji bila maji
Dar es Salaam. Katikati ya kilio cha ukosefu wa huduma ya maji safi na salama katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam, kumeibuka changamoto nyingine kwa wananchi kulalamikia kutumiwa ankara kubwa za huduma hiyo, hali inayowaathiri zaidi wa kipato cha chini. Hata hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira…