Yanga wenyeji, Simba wageni watatu

YANGA imewaweka nje wachezaji wapya wote, ikianza na kikosi chenye wenyeji huku Simba ikija na wapya watatu. Yanga inacheza dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii unaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwenye kikosi cha Yanga kilichoanza, hakuna ambaye amesajiliwa dirisha kubwa lililofungwa Septemba 7 mwaka huu. …

Read More

Othman awaahidi wavuvi Zanzibar mikopo, zana za kisasa

Pemba. Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameahidi kufanya mageuzi katika sekta ya uvuvi ikiwemo kuboresha miundombinu ya bandari na masoko ya samaki ili kuongeza kipato cha wavuvi. Othman amefafanua kuwa maboresho hayo yatawezesha wavuvi kupata sehemu nzuri za kuhifadhia mazao yao ili kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi….

Read More

Huduma jumuishi za kifedha zaipa BoT tuzo ya kimataifa

Dar es Salaam. Utekelezaji wa matumizi ya mfumo wa malipo ya papo kwa papo (TIPS) na matumizi ya msimbo namba (QR code) unaofahamika kama TANQR, umetajwa kuwa sababu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutunukiwa tuzo kuu ya ubunifu katika huduma jumuishi za fedha. Tuzo hiyo ijulikanayo kama Nestor Espenilla Jr. Financial Inclusion Innovation Award,…

Read More

Simba, Yanga zapishana dakika 12 kwa Mkapa

TIMU za Simba na Yanga tayari zipo ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaoanza saa 11:00 jioni. Yanga ndio imekuwa ya kwanza kufika hapa Benjamin Mkapa ikiwasili saa 9:22 alasiri, lakini ikashtua kidogo. Kilichofanyika, Yanga ikaibukia kusikojulikana ikitokea kwenye moja ya njia ya vumbi, kisha walinzi wake…

Read More

Kante, Pacome waibua presha Dabi ya Kariakoo

MUDA mchache kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii unaozikutanisha Yanga dhidi ya Simba, kuna presha iliibuka kwa mashabiki wa pande zote. Tukianza na Yanga, mashabiki wengi walianza kutishwa na taarifa kwamba kiungo wao fundi, Pacome Zouzoua hatakuwa sehemu ya mchezo huo. Hiyo ilitokana na Pacome kutoonekana kucheza mechi ya kilele cha Wiki wa Mwananchi…

Read More

Walioachiwa kwa kukutwa na meno ya tembo, wakutwa na hatia

Arusha. Mahakama Kuu Kanda ya Manyara imebatilisha uamuzi uliowaachia huru Meja Gidarge na Hussein Ally waliokuwa wameshtakiwa kwa kosa la kumiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria na kuwatia hatiani kwa kosa hilo. Juni 10, 2024 katika eneo la Kambini Kijiji cha Gijedaboung, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, watu hao walidaiwa kukutwa na meno ya…

Read More

Lissu aibua jipya kuhusu mashahidi wa Jamhuri

‎Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameibua hoja mpya dhidi ya mashahidi wa Jamhuri wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili, akidai kuwa ni hawastahili kisheria kufika mahakamani kutoa ushahidi kwenye kesi hiyo. Lissu ameibua madai hayo leo Jumanne, Septemba 16, 2025, katika mwendelezo wa usikilizwaji wa…

Read More