Profesa Mkenda: Hakuna zuio waliosomeshwa na Serikali kufanya kazi nje ya nchi
Dodoma. Serikali imesema ni ruksa kwa wanafunzi waliopewa ufadhili wa masomo ya sayansi nje ya nchi, kama watapata kazi huko baada ya kumaliza masomo ili mradi wapate kipato kinachoendana na ujuzi wao. Mbali na ruhusa hiyo, Serikali pia imewaita wadau wa elimu, benki, migodi na taasisi kwenye nia ya kusaidia ufadhili wa masomo ya sayansi…