Ubora wa makipa Azam wampa mzuka Ibenge
VIWANGO vizuri vinavyoonyeshwa na makipa watatu wa Azam, Aishi Manula, Zuberi Foba na Issa Fofana, vimempa matumaini makubwa ya kufanya vizuri kocha mkuu wa kikosi hicho, Mkongomani Florent Ibenge, katika michuano tofauti ya msimu huu. Katika mechi 15 za Ligi Kuu Bara ilizocheza Azam msimu huu, Manula ndiye anayeongoza kwa kucheza nyingi zaidi, akifanya hivyo…