ZEC yateketeza nyaraka 720,000 za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29
Unguja. Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemalizia kazi ya kuteketeza nyaraka 720,000 za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025. Kati ya nyaraka hizo 100,000 hazikutumika, zilizotumika Unguja ni nyaraka za kura 461,000 na Pemba kura 159,000. Akizungumza wakati wa kuteketeza nyaraka hizo leo Jumamosi, Februari 28, 2026 katika Shimo la Muungoni Mkoa wa Kusini Unguja,…