
Simulizi ya mwenyekiti wa mtaa aliyeongoza kwa miaka 39
Bukoba. Mkazi wa Mtaa wa Bulibata uliopo katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Alkadi Bagani (74) amekuwa mwenyekiti wa mtaa huo kwa kipindi cha miaka 39 sasa baada ya kuchaguliwa tena kwa miaka mitano ijayo. Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Novemba 29, 2024 baada ya kula kiapo cha utii na uadilifu wa uongozi, Bagani amesema…