RC CHALAMILA ATEMBELEA SOKO LA KAWE AMBALO LIMEUNGUA KWA MOTO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama Mhe Albert Chalamila ametembelea soko la Kawe ambalo limeungua moto usiku wa kuamkia leo Septemba 15,2025 kuwafariji wafanyabiashara waliopoteza mali zao kutokana na ajali hiyo ambapo ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kutoa kiasi cha shilingi milioni miamoja kama mkono wa pole Akizungumza mara baada ya kutembelea soko…

Read More

Watatu wafariki dunia kwa kuzama maporomoko ya Kipengele, wamo watoto wawili

Njombe. Watu watatu wakiwamo watoto wawili wamefariki dunia katika maporomoko ya maji ya hifadhi ya Mpanga Kipengele, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya. Kamanda wa Polisi mkoani Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa limetokea katika hifadhi hiyo iliyopo kata ya Mfumbi. “Hilo tukio nilikuwa silijui, lakini RCO hapa ndiyo ananiambia tukio hilo…

Read More

Waungana kusukuma ndoto ya Chato kuwa Mkoa

Geita. Mbunge wa zamani wa Chato, Dk Merdad Kalemani, na Deusdedith Katwale, wameahidi kushirikiana na wabunge wateule wa majimbo hayo kuhakikisha ndoto ya hayati Rais John Magufuli ya kuifanya Chato kuwa mkoa inatimia. Kalemani na Katwale, awatiania kugombea ubunge wa Chato Kusini na Kaskazini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), lakini kura hazikutosha. Machi 26, 2021,…

Read More

Kabutali kuanza kampeni wiki ijayo, aahidi kumaliza migogoro ya ardhi Mtumba

Dodoma. Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtumba kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Kayumbo Kabutali, ametangaza kuzindua kampeni zake Septemba 25, 2025, akieleza kuwa anakwenda kuchukua jimbo asubuhi, kwani siku zilizobaki kwa ajili ya kampeni zinamtosha. Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, alipoulizwa kwa nini hajaanza kampeni wakati pazia lake lilishafunguliwa tangu…

Read More

Dk Nchimbi awatumia ujumbe waliokosa uteuzi ndani ya CCM

Tanga. Mgombea mwenza wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi, amewataka wanachama wa chama hicho waliokosa fursa za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutulia na kuheshimu uamuzi wa vikao vya chama. Amejitolea mfano, akisema, mwaka 2005 jina lake lilienguliwa kwenye mbio za kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Tanzania,…

Read More

Soko la Kawe lateketea, Serikali yatoa neno

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa Soko la Kawe jijini Dar es Salaam, wamejikuta wakilala kwa majonzi baada ya soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, Jumatatu, Agosti 15, 2025, na kusababisha upotevu wa mali. Moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana, umeteketeza bidhaa mbalimbali walizokuwa wakitegemea kulipia mikopo kwenye taasisi za kifedha. Tukio hilo…

Read More

Sababu majanga ya moto majengo ya Kariakoo

Dar es Salaam. Kasi ya ukuaji wa biashara Kariakoo imeibua tatizo jipya la usalama baada ya kuibuka kwa matukio ya moto yaliyohusishwa na wapangaji kuhamia katika majengo kabla ya kukamilika. Ndani ya mwezi mmoja wa Agosti pekee, zimetokea ajali mbili za moto katika majengo yanayoendelea na ujenzi, huku kukiwa na wapangaji wanaoendelea na biashara zao….

Read More