Wateja 1,391 wa KCB walipwa amana zao
Dodoma. Bodi ya Bima ya Amana (DIB), imewalipa wateja 1,391 kati ya 2,797 wa Benki ya Wakulima Kagera (KCB), waliokuwa na amana chini ya Sh1.5 milioni. Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema hayo leo Jumanne Januari 28, 2025 wakati akijibu swali la Bernadeta Mshashu aliyehoji lini Serikali itawalipa wateja walioweka fedha zao katika benki…