
Sababu majanga ya moto majengo ya Kariakoo
Dar es Salaam. Kasi ya ukuaji wa biashara Kariakoo imeibua tatizo jipya la usalama baada ya kuibuka kwa matukio ya moto yaliyohusishwa na wapangaji kuhamia katika majengo kabla ya kukamilika. Ndani ya mwezi mmoja wa Agosti pekee, zimetokea ajali mbili za moto katika majengo yanayoendelea na ujenzi, huku kukiwa na wapangaji wanaoendelea na biashara zao….