Wawili waliohukumiwa kifo kwa mauaji, kujaribu kuua waachiwa huru
Arusha. Mahakama ya Rufani imebatilisha adhabu ya kunyongwa hadi kufa waliyohukumiwa watu wawili, baada ya kubaini kuwa ushahidi uliotumika kuwahukumu haukuthibitisha hatia yao bila kuacha shaka. Walioachiwa huru ni Emmanuel Sayi na Yohani Emmanuel, ambao awali, wao na watu wengine watano, walikutwa na hatia ya kumuua Ester Kondela na kujaribu kumuua Leticia Daud. Hukumu iliyowaachia…