Malasusa ataka Watanzania kuwa wasikivu kuelekea uchaguzi mkuu

Mwanga. Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Alex Malasusa, amesisitiza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uhaguzi mkuu, Watanzania wanapaswa kuwa wasikivu na kusikiliza kwa umakini, ili kuhakikisha nchi inaendelea kuimarika na kuwa na maendeleo endelevu. Malasusa ameyasema hayo leo, Mei 13, 2025, wakati akihitimisha ibada ya mazishi ya aliyekuwa Waziri…

Read More

Msigwa ataka mdahalo na Sugu uenyekiti Kanda ya Nyasa

Mbeya. Mgombea uenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa amesema mkakati wa chama hicho ni kupambana na kushinda katika uchaguzi ujao. Amesema iwapo atafanikiwa kutetea kiti hicho, atapambana kuhakikisha anapunguza udumavu uliopo katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini licha ya kuzalisha chakula cha kutosha. Msigwa amemtumia salamu…

Read More

WAZIRI ULEGA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU MIRADI YA BRT, AAGIZA IKAMILIKE KABLA YA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA.

Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, amefanya ziara ya kushtukiza usiku wa kuamkia leo Jumamosi tarehe 28, Disemba 2024 yenye lengo la kukagua maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo, Waziri Ulega ameagiza miradi hiyo ikamilike kabla ya msimu wa…

Read More

Faini zatawala Ligi Kuu Bara

KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) katika kikao cha Aprili 30, mwaka huu imepitia matukio yaliyojitokeza katika mechi za Ligi Kuu, Championship na First League na kutoa adhabu mbalimbali kwa timu na wachezaji.  Katika uamuzi uliotolewa timu ya Mashujaa imetozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la…

Read More

Huu hapa msimamo wa Malisa aliyetimuliwa CCM, asisitiza …

Dar es Salaam. Uamuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro kumfuta uanachama kada wake, Dk Godfrey Malisa umechukua sura mpya baada ya kada huyo kusema hatambui kilichofanyika. Makisa anayejiita kada mwandamizi wa CCM, amesema mpango wake wa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea…

Read More

Kitasa Fountain Gate kuibukia Namungo

UONGOZI wa Namungo, uko katika mazungumzo ya kupata saini ya aliyekuwa beki wa kati wa Fountain Gate, Jackson Shiga, ukiwa ni mwendelezo wa kusuka upya eneo la kujilinda, baada ya kuondoka kwa Erasto Nyoni na Mrundi Derrick Mukombozi. Nyota huyo alijiunga na Fountain Gate dirisha dogo la usajili msimu wa 2024-2025, kwa mkataba wa miezi…

Read More

Mapya yaibuka mahakamani kufungwa Kanisa la Askofu Gwajima

Dar es Salaam. Mvutano mkali wa kisheria, umeibuka kortini baada ya Serikali kuweka pingamizi la awali kupinga maombi yaliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Glory of Christ Tanzania linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima. Hata hivyo, katika uamuzi wake alioutoa Juni 6, 2025 na kuwekwa katika tovuti ya mahakama, Jaji Juliana Masabo wa Mahakama…

Read More