Mke wa Sumaye aibuka kidedea kortini

Kilimanjaro. Esther Frederick Sumaye ambaye ni mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, ameibuka kidedea katika kesi ardhi ya kugombea shamba namba 25 lililopo Madale eneo la Wazo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Ardhi aliyesikiliza kesi hiyo namba 99 ya 2023…

Read More

Wafanyabiashara Mbeya, Mwanza wakomaa na mgomo, Iringa nao walianzisha

Mbeya/Iringa/Mwanza. Wakati wafanyabiashara katika mkoa ya Mbeya na Mwanza wakiendelea na mgomo waliouanza jana, mkoani Iringa nako wamegoma. Mgomo wa wafanyabiashara hao wa maduka jijini Mbeya na Mwanza ulianza jana Juni 25, unalenga kuishinikiza Serikali kuondoa utitiri wa kodi na tozo mbalimbali ambazo si rafiki kwa wafanyabiashara. Leo Jumatano Juni 26, 2024, Mwananchi Digital ambayo…

Read More

Mawakili wa TLS kuwapa msaada wafungwa

Kilombero. Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Damas Ndumbaro amewahakikishia wafungwa katika magereza mbalimbali nchini, kuwa jopo la mawakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), litawafikia na kushughulikia changamoto zao za kisheria hususan rufaa. Akizungumza na askari pamoja na wafungwa katika Gereza la Kiberege, wilayani Kilombero, Dk Ndumbaro amesema kupitia kampeni ya Mama Samia Legal…

Read More

Waliostaafu Soko la Kariakoo kulipwa Sh306 milioni

Dar es Salaam. Jumla ya Sh306 milioni zinatarajiwa kulipwa na Shirika la Masoko Kariakoo  kwa madeni ya waliokuwa watumishi wa Soko la Kariakoo. Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa Aprili 18, 2025 na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, Hawa Ghasia wakati wa kikao cha Kumi cha Bodi hiyo kilichoketi jijini…

Read More

Serikali yazitaja hospitali zinazotoa tiba asilia

Dar es Salaam. Kama unasumbuliwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na unahitaji tiba za dawa za asili, Serikali imetaja hospitali 14 za mikoa ambazo tiba hizo hutolewa, ogopa matapeli. Hospitali hizo zimeongezeka kutoka saba ambazo Serikali, mwaka 2023, ilizitangaza kuanza kutoa huduma hiyo, sasa zimefika 14. Daktari humpima mgonjwa na kumweleza tatizo lake na…

Read More

EZY AUTO MOTORS YAONGEZA PUNGUZO MSIMU HUU WA SIKUKUU

Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji magari nchini ya Ezy Auto Motors Bi. Upendo Ngogo ameagiza watendaji wa mauzo katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka kuendelea kunufaisha wateja wao kupitia punguzo kubwa la bei sambamba na kutoa zawadi mbalimbali. Amesema hayo Novemba 29, 2024 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wafanyakazi wake…

Read More

Bado Watatu – 11 | Mwanaspoti

“AFANDE kama ulivyosema alama za dole gumba ni zile zile za kwanza. Hii imethibitisha kwamba muuaji ni mtu yule yule,” Ibrahim akaniambia kabla sijakaa kwenye kiti. Nilipokaa nikamuuliza: “Na zile alama za marehemu mmeshazichunguza?” “Tumezichunguza kujua kama ni mtu ambaye tuna rekodi naye lakini tumepata matokeo ya kushangaza kama yale tuliyoyapata mwanzo ndio maana nimekuita.”…

Read More