
Watoto wawili wa familia moja wafariki dunia kwa moto Tabora, mmoja akijeruhiwa
Tabora. Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa kwenye ajali ya moto katika eneo la Ikindwa, kata ya Mapambano, manispaa ya Tabora. Tukio hilo lilitokea asubuhi ya Septemba 13, 2025, ndani ya chumba wanacholala watoto hao, na mmoja kati yao alikuwa akichezea kiberiti na kisha kuwasha moto ulioshika kwenye godoro na kuwateketeza….