Maswali kutekwa mwanafunzi, kuuawa na mwili kuchomwa
Mbeya. Aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Mbeya, Shairose Mabula ameuawa kikatili kisha mwili kuchomwa moto, tukio lililoibua simanzi na maswali lukuki. Mwili wa mwanafunzi huyo ukitarajiwa kuzikwa kesho Jumamosi, Septemba 20, 2025, baba yake mzazi, Dk Mabula Mahande, amesimulia tukio hilo huku akiliomba Jeshi la Polisi kuongeza nguvu kuwabaini na kuwakamata waliohusika….