Watu 700 kutibiwa mtoto wa jicho Songwe

Mbeya. Zaidi ya wananchi 700 wakiwemo wazee waishio maeneo ya pembezoni mkoani Songwe, wanatarajia kunufaika na huduma uchunguzi wa mtoto wa jicho na upasuaji bure kwa lengo la kurejesha matumaini. Kambi hiyo iliyoanza leo Jumamosi Septemba 13 mpaka 19 mwaka huu, itahusisha madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) na Mkoa wa…

Read More

Mke wa diwani atokwa chozi la furaha akimnadi mume wake

Mbeya. Mke wa mgombea udiwani Kata ya Ruanda, Lydia Kibonde amejikuta akitokwa chozi la furaha wakati akimnadi mumewe, Isack Mwakubombaki na kutoa shukurani kwa wajumbe na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpitisha kugombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao. Lydia akizungumza leo Septemba 13, 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa mgombea huyo, amesema anawashukuru…

Read More

Wanunuzi wadogo wa Tanzanite walia mfumo wa ununuzi usio rafiki

Mirerani. Madalali wadogo na wakati wa madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wameiomba Serikali kutunga kanuni zitakazowawezesha kununua kila asilimia 20 ya uzalishaji wa madini hayo. Hatua hiyo itawawezesha kufanyika  magulio ya madini, pindi migodi ikizalisha tofauti na sasa inavyofanyika kwa hiari. Baadhi ya madalali hao wadogo wameyasema hayo leo…

Read More

Wauguzi, wakunga wakumbushwa kuzingatia maadili ya kazi zao

Tanga. Katibu Mkuu wa Chama Cha Wauguzi Tanzania, (Tanna), Geofrey Chacha amewataka wauguzi kuhakikisha wanazingatia kanuni na sheria za kazi zao, ili kuweza kuepukana na kashfa na tuhuma dhidi yao ambazo zinaweza kuwachafua kwenye taaluma. Akizungumza kwenye mkutano wa Chama cha Wauguzi Mkoa wa Tanga uliofanyika wilayani Muheza Jumamosi Septemba 13, 2025 kujadili mipango ya…

Read More

Albania yateua waziri roboti wa kupambana na ufisadi

Tirana. Albania imeweka rekodi ya dunia kwa kuwa nchi ya kwanza kuteua waziri aliyeundwa kwa akili bandia (AI), siyo waziri wa teknolojia ya AI, bali waziri halisi wa kidijitali, aliyeundwa kwa misimbo na kuendeshwa na mfumo wa kisasa wa akili bandia. Jina lake ni Diella, linalomaanisha ‘mwanga wa jua’ kwa Kialbania ndilo jina la roboti,…

Read More

MPINA ATEULIWA NA TUME KUWANIA URAIS 2025

  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi nakala ya fomu za uteuzi kwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT – WAZALENDO), Mhe. Luhaga Joelson…

Read More