PIGABET YAWAZAWADIA WASHINDI KUPITIA KAMPENI ZA KILA WIKI

 Dar es Salaam  Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Pigabet imeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake kupitia kampeni kabambe zinazofanyika kila wiki kwa wateja nchini kote. Katika hafla ya hivi karibuni, Hemed Misonge, mhudumu kutoka Pigabet, aliungana na washindi wa promosheni hizo kwa kuwapatia zawadi nono zikiwemo: Smartphone Samsung Galaxy A26 5G kupitia…

Read More

Msukuma afichua kilichomuondoa Bulaya CCM

Bunda. Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Kasheku, maarufu Msukuma amesema majungu ndani ya chama hicho ndiyo yaliyosababisha mgombea ubunge Bunda Mjini, Ester Bulaya kuhamia upinzani. Msukuma ameyasema hayo mjini Bunda leo Jumamosi Septemba 13, 2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za chama hicho jimboni humo, huku akiwataka wakazi wa jimbo hilo kukipigia…

Read More

Samia kuifanya Kigoma kitovu cha biashara na nchi jirani

Kasulu. Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwavutia zaidi wawekezaji kwenda kuwekeza Kigoma ili kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika na nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Samia amebainisha hayo leo Septemba 13, 2025 wakati wa mkutano wake wa…

Read More

MGOMBEA UBUNGE CCM CHATO KASKAZINI KUANZA NA SOKO KUU

Mgombea Ubunge kupitia CCM Jimbo la Chato Kaskazini akiomba kura kwa wananchi.Mgombea Ubunge Jimbo la Chato Kaskazini, Mwl. Cornel Magembe,akiomba kura kwa wananchi wa Jimbo hilo. …….. MGOMBEA Ubunge Jimbo la Chato Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwl.Cornel Magembe, ameahidi kuanza na ujenzi wa soko kuu la wilaya ya Chato mkoani Geita iwapo atachakuguliwa…

Read More

Mabinti wa Dhahabu wapewa heshima kwa kutwaa Kombe la Dunia

BAADA ya kufanikisha historia isiyosahaulika, wachezaji wa kike wa Tanzania waliowakilisha taifa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia kwa watu wasio na makazi, wamepatiwa pongezi za heshima. Mashindano hayo yalifanyika Agosti mwaka huu nchini Norway, ambapo mabinti hao waliweka rekodi mpya ya kimataifa. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo kwa upande…

Read More

Kauli ya Mpina baada ya kupitishwa INEC

Dar es Salaam. Mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amesema ataanza na hotuba ya saa sita ili Watanzania waijue nchi yao kikamilifu, kabla ya kutumia siku 45 za kampeni zilizobakia. Amesema kinachofuata baada ya kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ni kuzindua ilani, kueleza maono ya mgombea na uzinduzi…

Read More

DP kuungana na CUF Uyole, mgombea awaita CCM na Chaumma

Mbeya. Wakati Chama cha Democratic Party (DP) kikitangaza kumuunga mkono mgombea ubunge Uyole, Ibrahim Mwakwama wa Chama cha Wananchi (CUF), mgombea huyo amesema matarajio yake ni vyama vyote kumnadi kutokana na kukubalika kwa jamii. DP walitarajia kufanya mkutano wake wa kumnadi mgombea urais, Abdul Mluya mkoani Mbeya, lakini ziara hiyo haitakuwapo kutokana na dharura, badala…

Read More