KONA YA MZAZI: Mzazi muwekee mipaka dada wa kazi malezi ya mtoto
Katika familia nyingi hivi sasa hasa zinazoishi mijini, wazazi hulazimika kuajiri wasaidizi wa nyumbani ili kusaidia kazi za kila siku, ikiwamo malezi ya watoto. Hali hii inatokana na majukumu ya kikazi na shughuli nyingi zinazowakabili wazazi hao. Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa msaada huo, ni wajibu wa mzazi kuweka mipaka iliyo wazi kuhusu nafasi…